VIONGOZI WA DINI NA MILA WAANDAMANA WALITAKA BUNGE KUTUNGA SHERIA YA KUPINGA USHOGA.

WATAKA RAIS SAMIA KUKAZA ZAIDI YA MUSEVEN ILI WAZUNGU WAJUE AFRIKA SIYO PAKUCHEZEA. 

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Viongozi wa madhehebu ya dini mbali mbali Jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania wameandana kwa dhumuni maalum la kupinga ushoga, ulawiti pamoja na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watototo wadogo.


Maandamano hayo ya amani yaliyo udhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe, John Mongela, yamepelekea viongozi wa dini kulitaka Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutunga sera na kusainiwa na Rais ili kuweza kuwa sheria ya kupiga mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

Wakiongozwa na viongozi wakuu wa madhebu hayo kutoka dini ya kiislam na kikrsto kwa pamoja wamelitaka Bunge la Tanzania kuto kukaa kimya na kuacha swala la kupinga ushoga libaki kwa viongozi wa dini na mila.

"Maandamano pekee haitoshi Nimuombe Rais kutunga sheria ambayo itapitishwa na bunge ili watakao bainika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria, Aungane na Rais wa Uganda ili hata wao pia wataona Afrika imekataa na inapinga ushoga". Amesema Dkt, Yoseph Nyambega Otieno, Mchungaji wa kanisa la WASABATO.


"Tunaomba Bunge nalo litoe tamko juu ya jambo hili maana tuona hao mashoga, wasagaji wanaendelea kuwa katikati yetu, katika jambo hili hatu hitaji msaada kutoka nje sisi tunatosha tunaomba Bunge la Tanzania sasa liongee. Kuyaacha matumizi ya mwanamke ya asili na kwenda katika matumizi ya kinyume basi wote ni wadhambi na adhabu yake ni kupigwa hadi kufa". Aliongeza Mchungaji Dkt, Yoseph Nyambega.

Aidha Dkt, Nyambega alisema kuwa katika jambo la mapenzi ya jinsia moja lina fanya uchechefu kwa mwanadamu, Mwanaume kulala na mwanaume mwenzie kwanza ni kusambaza magonjwa pili ni kuto kuongeza familia maana hakuna mwanamke anazaa mtoto na mwanamke mwenzie wala mwanaume anaye zaa na mwanaume mwenzie.

Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Arusha Shekhe, Shaban Bin Juma, amesema kwamba Kulinda kizazi au uzao wa watanzania ni kutoa mafundisho ambayo hayapingani na mwenyezi mungu.


"Tukilinda imani tusichanganye na kitu chochote, sasa katika maandiko hakuna neno ushoga kwa maana hiyo usoga ni wakupinga na kuukemea kwa nguvu zote maana siyo neno la mwenyezi mungu, Misuko suko iliyo iandama dini ni mingi hasa swala ndoa ya jinsia moja, ulawiti na usagaji, Jambo hili lisipo kemewa na kulikataa tuta alibikiwa watanzania wote".Amesema Shekhe Shaban Bin Juma.

"Sisi kama watanzani yatupasa kuungana kwa pamoja ili kutokomeza haya, Tushirikiana na vyombo vyetu vya dora kuhakikisha wote wanao husika na matendo haya wafikishwe katika vyombo vya sheria ili kupata stahiki za maovu yao". Aliongeza Shekhe Shaban Bin Juma.


Aidha Shekhe Abubakari aliwataka watanzania kutilia mkazo gharika la ushoga lisije likawakumba kwa pamoja maana halita angalia nani ni nani na kusisitiza kwamba jambo la ushoga wasilikubali kuwa wanavyo ambiwa haki ya ubinadamu.


"Wazazi wote tuhakikishe huu mpango wa kutafuta maendeleo na kumkabidhi kwa mtoto kwa mtu usiye mjua akulele ifike mahali tuachane nao, tusiwapeleke watoto wadogo kwenye shule za bweni maana haya yote wanaenda kuyaokota huko maana mwalimu siyo ndugu yako wala hana uchungu na mwanao". Amesema Shekhe Shabani Bin Juma.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT ) Arusha Mjini kati Solomon Masangwa ambaye alieleza tamko la haki ya Amani katika maandamano hayo na kumuomba Rais wa Tanza Samia Suluhu Hassan kufanya kama alicho fanya Rais wa Uganda Rais Yoweri Kaguta Museven juu ya kuweka sheria kali ya kuoinga ushonga.


"Tusiukaribishe utamaduni huo wa kigeni maana tutakuja kuishia mahalai pabaya maana hakuna ongezeko la mwanandamu linalo tokana na mapenzi ya jinsia moja niwazi kwamba mpango huo wa ushiga ni kufuta mpango wa mwanadamu kuzaliana kama lilivyo agiza neno la mungu " Enendeni Mkaujaze ulimwengu". Amesma Askofu Masangwa.


"Tamko letu la Haki ya Amani ni kila mmoja asimkaribishe mgeni yeyeote asiye ijua familia yake, na sisi kama waafrika tumunge mkono Rais wa Uganda Mhe, Museven kwa kupinga mapenzi ya jinsia moja, ulawiti na ushoga na Tunamuomba Rais wetu mpendwa kufanya kama alicho kifanya mseni ili hata wao wazungu wajue Afrika siyo ya kuchezea". Aliongeza Masangwa.

Kwa upande wao viongozi wa kimila waliyoshiriki maandano hayo ya amani ya kupinga ushoga walieleza kuwa wao kama viongozi wa kimila hawata aacha mila zao kiafrika zipotee kwa mambo ya utandawazi wa kigeni na kueleza hwataacha kutoa adhabu za kimila endapo watabaini katika koo zao zinajihusisha na swqla zima la ushoga.

Olekisongo Mejo ni Kiongozi wa kabila la maasai nchini Tanzania. ameeleza kwamba lawamba kubwa zipelekwe kwa wazazi kwa kuwaacha watoto wao kuacha mila na dini za Kiafrika ndiyo maana hawa wanafuta tamaduni za waalibifu wa kigeni na wanapata nafasi ya kuharibu watoto wao.


"Watoto hawa hawajui chochote ila mazingira ambayo mzazi unamuacha kwa kigezo cha kutafuta pesa hii siyo ya kufumbia macho na huko makanisani na misikitini tuungane kwa pamoja kwa kuelemisha jamii zetu ziendeleze utamaduni wetu kama watanzania na waafrika kwa ujumla". Amesema Laigwanani Meijo.


"Sisi kwetu wamasai tumepitisha kwa atakaye bainika kujihusisha na ushiha atadhibiwa viboko 70 akiendelea na hizo tabia ni kumaliza kabisa na kumuondoa duniani ili kama ni sisi viongozi tufungwe kuliko hawa wanaofanya tukio hilo badae wanarudi tena mtaani kuendeleza ubaya kwa vijana wetu". Aliongeza Laigwani Meijo.

Naye Kiongozi wa kabila la wameru Mshiri Ersom Sumari, ameeleza kwamba kwenye mila zao ushoga hauna jina na kutokana na mila zinavyo kataza kama kitu jakina jina wasifuatane nacho na kuitaka serikali kupitia upya shuke zote za binafsi maana ndizo zinaongoza kwa kulaumiwa.


"Niombe Serikali kuangali usajili wa shule binafsi ndizo zinaongoza kwa ulawiti wa watoto wadogo kwa kigezo cha kuwalea watoto hao na kupekea misaada kadha wa kadha kutoka nje kwa watu wanao waita ni wadhamini kwa watoto".Amesema Mshiri Sumari.


"Katika swala la ushoga kwa upande wa Meru tumepitisha kuchapa fimbo 70 kwa atakaye bainika kufanya vitendo hivyo ikiwemo ulawiti pasipo kuangali haki za binadamu maana haya ndiyo yanaleta ukakasi mkubwa kwa kusema haki za binadamu na dunia inaangamia". Aliongeza Mshiri Sumari.

Awali Kamanda wa Polisi wilaya ya Arusha ( OCD ) ASP George Malema Kila siku makosa ya ulawiti hayapungui matatu na wahanga wakubwa ni watoto wa shule za msingi, ktokana na uchunguzi na upelelezi wa kina waliyo ufanya wamegundua madhara hayo yanaanzia shule za msingi.


"Mambo haya yamekuja kwa maandalizi ya watu fulani na sisi tulififishwa tukijua ni imani ya kishirikina na sasa tunafumbuliwa na kujua haya yanayo fanyika sio ushirikina bali ni vitu vya kumaliza kizazi na taifa lisiwe na vijana tegemezi". Alisema OCD Malema


"Kwa takwimu za nchi Arusha ni Mkoa wa 3 kwa ukatili wa kijinsia na matukio ya ulawiti wa watoto wadogo, na haya yote yanaanzia shuleni niwaombe viongizi wenye dhamana kuzichukulia hatua kali shuke hizi maana mpaka sasa zipo shule zenye upinde ambao unahamasisha ushoga hayo yote ni kutokana na misaada mbali mbali wanayo ipata pasipo kujali watoto wetu wanaathirika". Ameonheza OCD Malema.

Akipokea maombi ya viongozi wa madhebu mbali mbali ya dini pamoja na viongozi wa mila wakimuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutunga sheria ya kupinga ushoga, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alieleza kwamba atafikisha maombi hayo kwa Rais Samia.

Rc Mongela ameeleza kwamba Kunahatari kubwa sana kwa vijana na kuna mashule bado wanafundiaha watoto maswala ya ushoga na kueleza kwamba kwa sasa kuna namna nyingi ya kutafakari maana waafrika walitaka kuzubaishwa kwa mambo ya ushoga,ulawiti kwa watoto na mauaji kuwa ni ushirikina.


"Kwangu mimi naamini huu ni mpango maalum ulipwangwa na wengine huko duniani, Ujumbe huu mimi nitaufikisha kwa Mhe, Rais. Dkt, Samia Suluhi Hassan ili yeye kama kiongozi wetu mkuu atupe dira ya pamoja kama taifa". Alisema Mongela.

 "Pia kwa mkoa wetu wa Arusha hadi sasa kesi zaidi ya 200 za ulawiti na unyanyasaji zimetolewa hukumu na hatua kali zimeshachukuliwa, Kwa gharama yeyote ile tusivumilie vitendo vya unyanyasaji iwe kwa wanawake wala kwa watoto, kuna hatari kubwa sana kama watoto wa kiume kuharibiwa". Aliongeza Mongela.


"Wazazi niwaombe sana watoto wa kiume ndiyo wamelengwa zaidi katika ulawiti na kwa jinsi ya mila na desturi zetu bado tunawatengea wanaume katika ibada na mambo mengine mengi endapo wataharibiwa tutakuwa na viongizi wengi mashoga". Alisisitiza Mongela.

Aidha Rc Mongela aliwataka wazazi kusimamia tabia ya kufanya kazi kwa watoto wao na vijana ili kujenga na kuandaa kizazi kinacho fanya kazi na kupenda kazi ili kuacha kupenda vya kupewa kutoka kwa wazazi kitu ambacho kinaweza kuhatarisha ushawi wa maisha yao.


"Kuna vijana wengi hadi sasa tegeo meo kubwa la vijana hao ni wazazi leo hii mzazi akiondoka anashindwa kujua aanzie wapi na ndiyo mwanzo wa haya yote yanapo anzia kuingia katika mambo kadha wa kadha". Amesema Mongela

"Serikali haitafumbia macho jambo hili na tutaendelea kuunga mkono jumuiya hii ya amani kwanza pamoja na jumuiya ya malidhiano na kwa kupindi chote, Mimi niwahaidi toka uongozi wa nchi hii madhehebu yetu ya dini yamekuwa sehemu ya utulivu katika nchi yetu". aliongeza Mongela.

Comments