DKT SAMIA NA DKT MWINYI KUTIKISA ARUSHA KWA SIKU 3.

NI KATIKA MAPAMBANO ZIDI YA RUSHWA AFRIKA, HUKU TANZANIA IKIADHIMISHA MIAKA 20 YA MKATABA.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Picha ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya maadhamisho ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika itakayo fanyika tatehe 11.7.2023 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Julai 6,2023 Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na maonyesho kwa siku 3 kuanzia tarehe 9, 7. 2023 ambapo yatafunguliwa na Rais wa Zanziba Dkt, Hussein Ali Mwinyi.

Picha ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt, Hussen Ali Mwinyi.

"Siku ya Mapambano dhidi ya Rusha Barani Afrika huadhimishwa Julai 11 ya kila mwaka tangu ilipoazimishwa mwaka 2017 na kwa mwaka huu 2023 Tanzania imepewq heshima ya kuwa nchi mwenyeji wa maadhimisho haya". Amesema Rc Mongela.

Mongela ameeleza kuwa siku ya tarehe 9 ambayo ndiyo siku maadhimisho hayo yatafunguliwa na Dkt Mwinyi yatatanguliwa na maandano kuzunguka mji wa Jiji la Arusha na kisha kufunguliwa katika ukumbi wa AICC siku hiyo hiyo.


"Siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya kupambana na Rushwa barani Afrika yatakayo fanyika Julai 11,2023 mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasaan na tushukuru kuona fahari kubwa ya kupokea ugeni mkubwa koka bara la Afrika katika maadhimisho haya". Amesema Rc Mongela.


Sanjali na hayo Mongela ameeleza kuwa siku ya mapambano dhidi ya rushwa Afrika toka kuanzishwa mwaka 2003 Tanzania inaadhimisha miaka 20 ya utekelezaji wa mkatqba wa umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa (AUPCPCC) ambapo mkataba huo ulisainiwa kwaka 2003.

"Katika maadhimisho haya tunatarajia kuwa na wadau mbali mbali wa ndani ya nchi na nje ya Tanzania wakiwemo viongozi na watumishi wa taasisi za serikali, mashirika ya umma pamoja na wakuu wa mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa Afrika pia washiriki wengine ni wanasiasa, wawakilishi wa mabalozi, viongizi wa dini, wajumbe wa AUBC". Amesema Mongela.


Aidha Mongela amesema kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutoa nafasi kwa nchi wanachama kutafakari juhudi za mapambano dhidi ya rushwa ili kuweza kuchukua hatua stahiki, kuboresha na kuimarisha mapambano hayo.

Pia Mongela amewahakikishia wageni wote amani na utulivu wakati wote watakapo kuwa Jijini Arusha na kueleza kuwa Arusha iko salama na ulinzi umeimalishwa vya kutokasha kila pembe ya Jiji la Arusha.


Kuelekea maadhisho hayo ya kudhibiti na kupambana na Rushwa Afrika yanaongezwa na kaulimbiu isemayo "Mafanikio baada miaka 20 ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia na Kupambana na Rushwa na matarajio yake".

Comments