MWENGE WA UHURU WAFIKA NYUMBANI KWA SOKOINE.
MJANE WA SOKOINE AISHUKURU SERIKALI KUENDELEA KUMKUMBUKA.
Na Lucas Myovela - MONDULI, ARUSHA.
Monduli: Mwenge wa Uhuru umefika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine leo Julai mosi 2023.
Akiongea na Mjane wa Sokoine kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg, Abdallah Kaim Shahib amesema wao kama viongizi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2023 wamefarijika kufika na mwenge wa uhuru nyumbani kwa miongoni mwa waasisi wa Taifa la Tanzania.
Pia viongozi hao wameza kuweka mashada katika kaburi la Hayati Sokoine pamoja na kutoa mkono wa pole kwa mjane pamoja na familia hiyo na kuwaomba waendelee kuwa wazalendo na kulipambania Taifa kama alivyo kuwa hayati Sokoine.
Hata hivyo Jumla ya Miradi 14 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.8 wilayani Monduli Mkoani Arusha, imezinduliwa ,kuwekwa mawe ya msingi ,kutembelewa na mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ukiwemo mradi wa maji wa sh,milioni 500.7 katika kata ya Meserani.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Ndg, Joshua Nasari wakati wa makabidiano ya Mwenge wa Uhuru leo Julai 1, 2023 katika eneo la Meserani, ukitokea jijini Arusha, ambapo alisema kuwa miradi hiyo inatekelezwa na fedha kutoka serikali kuu,Halmashauri na nguvu za wananchi
Alifafanua kuwa miongoni mwa fedha hizo kiasi cha sh,bilioni 1.17 ni kutoka serikali kuu sh,milioni 30 kutoka halmashauri na nguvu za wananchi shilingi milioni 600.
Akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Meserani Bwawani, kata ya Meserani , wenye thamani ya shilingi milioni549,780,722 utakao hudumia wakazi wapatao 4752,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Abdalah Shaib Kaim alipongeza mradi huo kwa kukidhi ubora na matumizi sahihi ya fedha za umma yanayoendana na thamani ya mradi na kusisitiza kuwa lazima utekelezaji wa miradi uzingatie uzalendo wa kweli.
"Ndugu zangu wana Monduli niwapongeze sana kwa mradi huu mkubwa kwani umezingatia ubora, vigezo vyote vinavyotakiwa ikiwemo nyaraka sahihi za mradi ,nyinyi ni wazalendo wa kweli" alisema Shaib.
Naye meneja wa mamlaka ya maji Monduli, RUWASA, ,mhandisi Neville Msaki ,alisema mradi huo pia utahudumia vijiji jirani vya Engorika,Lengiloriti na Moita Kiloriti na unatekelezwa na fedha kutoka serikali kuu .
Naye mbunge wa Monduli, Fredy Lowasa, alimpongeza rais Samia suluhu Hassan kwa kupeleka fedha jimboni kwake zilizofanikisha kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo ukiwemo mradi mkubwa wa maji ambayo imezinduliwa na mbio za mwenge.
Alisema Rais Samia aliahidi kutoa fedha kiasi cha sh,bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji kutoka Ngaramtoni wilaya ya Arumeru, utakaohudumia vijiji 13 na hivyi kuondoa changamoto ya maji kwa kiasi kikubwa katika jimbo hilo.
"Namshukuru Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo jimbo la monduli ". amesema Fred Lowassa.
Mwenge wa uhuru, pia umezindua miradi mbalimbali ya Zahanati,Madarasa,vikundi vya vijana,barabara ya Lami,chanzo cha maji na klabu ya kikundi cha vijana wapinga rushwa wapatao 50 katika chuo cha maendeleo ya jamii Monduli.
Comments
Post a Comment