SITA WADAKWA KWA KUUWA SIMBA NA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO.

NI BAADA YA KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA MAJANGILI KUPIGA MSAKO USIKU NA MCHANA BAADA KUPATA TAARIFA FICHE KUTOKA KWA RAIA WEMA.

Mwandishi wetu- Babati.

Watu sita wamekamatwa kwa kujihusisha na matukio ya ujangili katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge,wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,watatu wakinaswa na vipande sita vya meno ya Tembo na wengine kwa kuuwa Simba.

 Watuhumiwa hao ,wamekamatwa na kikosi maalum Cha Kupambana na ujangili Burunge WMA ,kinaundwa na Askari kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA), Askari wa Burunge WMA,Halmashauri ya Babati, Askari wa doria wa chemchem association na Jeshi la polisi.


Kukamatwa wa watuhumiwa hao, sita kumetokana na uchunguzi, uliofanywa na kikosi hicho baada ya kupata taarifa za watuhumiwa kutafuta wateja wa kununua meno ya Tembo lakini pia baada ya kubaini kuuawa kwa simba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara,George Katabazi alithibitisha jana kukamatwa watuhumiwa hao sita na kueleza uchunguzi, bado unaendelea ili kubaini mtandao wao.


"Bado tunaendelea na uchunguzi kujua mtandao mzima wa biashara hii ya Meno ya Tembo na uchunguzi ukikamilika baada ya kuwakamata watuhumiwa wote taarifa itatolewa"alisema RPC KATABAZI


Watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kukutwa na vipande sita vya meno ya Tembo ni Said Magodoro(45) mkazi wa Magugu Babati,Juma Ismail(44) mkazi wa Kondoa na Issa Hussein(58) mkazi wa Kondoa pia.


Habari za uhakika toka kikosi hicho, zimebaini watuhumiwa hao, walikamatwa Julai 4 mwaka huu,kijiji cha Matufa wilayani Babati saa tisa usiku.

"Watuhumiwa hao, tuliwakamatwa kutokana na taarifa kutoka kwa wasiri wetu kuwa wanamiliki meno ya Tembo na walikuwa wanataka kuyauza "alisema Afisa mmoja katika kikosi hicho maalum.


Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumetokana na mafunzo mazuri ambayo walipata ya kukabiliana na ujangili, ambayo yalitolewa na TAWA kwa ushirikiano na Chemchem Association .


Katika msako huo, pia watuhumiwa watatu walikamatwa baada ya kuuwa simba kwa kumchoma mishale, wakilipiza kisasi Simba kula Ng'ombe.


Akizungumzia matukio ya ujangili, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TAWA kanda ya Kaskazini,Peter Mbanjoko alionya baadhi ya watu, kujihusisha na ujangili kanda ya kaskazini, kwani lazima watakamatwa.


"Tutaendelea kuwakamata wote ambao wanajihusisha na ujangili na kama wanataka wabaki salama waache hivi vitendo, ikiwepo pia kuuwa wanyama"alisema


Mbanjoko alisema TAWA kwa kushirikiana na vyombo vingine, wameimarisha doria katika maeneo yote nje ya hifadhi za Taifa ili kuhakikisha watu wachache ambao wanajihusisha na ujangili wanakamatwa.


Kamishna msaidizi wa TAWA kanda ya kaskazini,Privatus Kasisi aliwataka wakazi wa eneo la Burunge WMA, kutoa ushirikiano kwa TAWA na vyombo vingine ili kuhakikisha wanaojihusisha na ujangili wanakamatwa.


Kasisi alisema TAWA itaimarisha ulinzi katika eneo hilo, ikiwepo pia kusaidia kudhibiti ongezeko kubwa na matukio ya wanyama wakali na waharibifu kuingia katika maeneo ya wananchi.

Simba aliye uwawa na majangili hao katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge,wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.
Hawa ni baadhi ya majangili hao sita waliyo kamatwa katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge,wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

Comments