ALIYE KUWA MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA AFUNGWA JELA MIAKA 20.

 KATIBA MPYA KUANZA KASI, SIYO TENA KUSUBILI.

SIRI NZITO KIFO CHA BILIONEA WA MADINI NA MWANAE.


VICHWA VYA HABARI VIKUBWA MAGAZETINI LEO SEPTEMBER 1, 2023. KUTOKA MOTIVE TV.












HABARI YA KUHUKUMIWA PIMA.



ARUSHA: Mahakama ya hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha dkt John Pima na wenzake wawili kwenda jela kutumikia kifunga cha miaka 20 baada ya kukutwa na hatia ya makosa 9 ya uhujumu uchumi .

Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu Saraphina Nsana katika kesi namba 5 ya mwaka 2022 ya uhujumu uchumi.

Wengine waliohukumiwa kifungo cha miaka 20 kila mmoja ni Mariam Mshana aliyekuwa mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, na innosenti Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo hakimu Nsana alisema kuwa mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili imejidhisha pasipo shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka na kuwatia hatiani.

"Kwa kuzingatia ushahidi huo na kwamba kama washtakiwa wanarekodi ya makosa ya jinai ,na utegemezi wa familia mahakama inawahukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja na iwapo kama hamjaridhika na adhabu hiyo nafasi ya kukata rufaa ipo wazi".

Hata hivyo bado Dk. Pima na wenzake wanakabiliwa na kesi nyingine mbali na kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi ,namba tano ya mwaka 2022.

Comments