BREAKING NEWS: RAIS SAMIA AMEFANYA MABADILIKO YA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU.

DKT, DOTTO BITEKO ALAMBA UNAIBU WAZIRI MKUU.

Na Lucas Myovela.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suhulu Hassan, Leo Agosti 30, 2023, amefanya mabadiliko madogo ya Mawqziri pamoja na Makatibu wakuu huku.


Miongoni Mwa mabadiliko hayo ni kuwapandisha waliyo kuwa Manaibu Mawaziri na kuwa Mawaziri kamili huku wengine wakihamishwa wizara zao.

Pia Rais Samia amemteua kwa mara ya kwanza Dkt, Dotto Biteko, kuwa  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Katika Nafasi ya Naibu Waziri Mkuu atakuwa anashughulikia Uratibu wa Shughuli za Serikali.


Ikumbukwe nafasi hii ya Naibu Waziri Mkuu kwa mara ya kwanza aliteuliwa Marehemu Agostino Lyatonga Mrema mnamo mwaka 1993, ili kuongezewa nguvu katika nafasi yake aliyekuwa nayo ya Waziri wa Mambo ya ndani chini ya Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi.


Pia Ras Samia Amemhamisha January Makamba kutoka Wizara ya Nishati na Kwenda Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


MKEKA KAMILI WA MABADILIKO MADOGO BARAZA LA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU.






Comments