RAIS SAMIA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA WANAJAMBO ZITO KESHO ARUSHA.

 NI UFUNGUZI WA KWANZA WA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI NA WAKURUGENZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA SERIKALI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Picha ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ( Picha na Maktaba ).

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa Kufungua kikao kazi cha wenyeviti na Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma pamoja na Taasisi za kiserikali, Pia anatarajiwa kuhudhuria kwenye kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya kanisa la KKKT ambapo matukio yote hayo yatafanyika Jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela Mapema leo Agosti 18, 2023, amesema kuwa Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan, Mnanmo tarehe 19/8/2023, atafungua kikao kazi cha Wenyeviti na Wakurugenzi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali,utakaofanuika Ukumbi wa mikutano ya kimataifa, AICC Jijini Arusha.


Pia Mongela ameeleza kuwa kuwa tarehe 21/8/2023, Mhe, Rais Samia, atakuwa mgeni rasmi kwenye madhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la kiluthelu Nchini, KKKT yatakayofanyika kwenye Chuo cha Makumura,kilichopo Makumura Wilayani Arumeru.


Aidha Mongela ameongeza kuwa mbali na ugeni huo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani viongozi wenheni watakao kuwepo ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dkt Tulia Acksoni pamoja na mawaziri mbali mbali.

"Kwa upande wa maandalizi yote yamekamilka kwa upande wa ulinzi na usalama, Pia niwaombe wana Arusha tuendelee kushirikiana kwa pamoja kudumisha amani na uoendo wetu kama watanzania pindi viongozi wetu watakapo kuwa hapa Mkoani kwetu". Amesema Mongela.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la mashirika ya umma na Taasisiza Serikali Ndg, Sabasaba Moshingi, amesema kuwa Mhe, Rais anafungua kikao kazi cha kwanza kufanyika kwa watumishi hao huku lengo la kikao hicho ni kuziwezesha Taasisi na mashirika kutengeneza faida na kutoa huduma bora na nzuri.


"Jumla ya taasisi 248 yakiwemo mashirika ya umma na Taasisi za Serikali yatashiriki kikao hicho ambapo wajumbe zaidi ya 1000 watashiriki katika kikao hicho, Pia katika kikao hiki tutaongizwa na kauli mbiu isemayo "Mwelekeo mpya wa usimizi na uendeshaji wa Taasisi za umma". Amesema Moshingi.


Awali Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano ya kimataifa AICC Ndg, Ephraimu Mafuru,amesema nchi yetu imefikia ya nafasi ya tano barani Afrika Kwa kuandaa mikutano ya Utalii kimataifa .


Ameeleza kuwa nchi ambazo zimetutangulia ni Afrika kusini,Moroco,Rwanda,na Misri,na bado nchi yetu inaendelea kufanya vizuri kwenye Uchumi wa mikutano ya kimataifa na Katika kipindi cha miaka mitano ijayo tunaweza kufikia nafasi ya tatu bora.

"Nchi yetu ni mwanachama wa Taasisi ya ICA,ambayo ni Taasisi inayoandaa mikutano mikubwa inayofanyika barani Afrika,na Kila mwaka AICC,inapokea taarifa kutoka kwenye Taasisi hiyo imefikia nafasi ya ngapi Katika kuandaa mikutano ya Uchumi wa utalii". Amesema Mafuru.


Pia ameleza kwamba  mwaka 2019 Katika mikutano iliyofanyika barani Afrika nchi yetu iliweza kuandaa mikutano 19 ambayo ni sawa na asilimia 30% ya mikutano yote inayoaandaliwa na Taasisi hiyo.


"Mwaka 2022 nchi yetu ilifanikiwa kuandaa mikutano 18 iliyofanyika barani Afrika na mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia,ya kufungua nchi na tupo kwenye Uchumi wa mikutano". Amesema Mafuru.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Viongozi mashirika ya umma na Taasisi za Serikali ,Latifa Mohamed Hamisi,amesema kuwa wanatarajia kupata mwelekeo mpya wa usimamizi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali Katika kutoa huduma bora na baada ya kikao hicho kutakuwepo na mabadiliko makubwa ya utendaji ma usimamizi wa mashirika hayo na Taasisi za Serikali.


Comments