ANDIKO LA WAZI LA GODBLES LEMA KWA RAIS DKT, SAMIA BAADA YA JESHI LA POLISI KUZUIA MKUTANO WA CHADEMA LOLIONDO WILAYANI NGORONGORO MKOANI ARUSHA.

ANDIKO LA WAZI LA GODBLESS LEMA KWA RAIS DKT, SAMIA BAADA YA JESHI LA POLISI KUZUIA MKUTANO WA CHADEMA LOLIONDO WILAYANI NGORONGORO MKOANI ARUSHA.

Na Lucas Myovela @Motive Tv

Mwanasiasa Mkwengwe na Mbobezi wa maswala ya siasa hapa nchini Godbles Lema, ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ameandika andiko kupitia mtandao wake wa twiter akimuomba Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzani Mhe, Samia Suluhu Hassan kupitia maandiko matakatifu katika Biblia takatifu.

Lema Kupitia Mtandao wake wa Twiter amemuomba Mhe, Rais kusoma Kitabu kitakatifu cha Biblia na hasa katika kitabu cha Wafalme 2.7.


Lema ameandika hayo baada ya Jeshi la Polisi kutoa barua ya kuzuia Mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA uliyokuwa ufanyike tarehe 8 na 9 mwezi huu wa Septemba 2023 katika eneo la Longido katika tarafa ya Ngorongoro, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.


ANDIKO KUTOKA KWA GODBLES LEMA KUPITIA UKURASA WAKE WA TWITER.

"Mhe, Rais najua wewe sio muhumini wa dini ya Kikrsto, lakini Pata muda soma this very interesting article kktk Biblia,Wafalme 2: 7.Soma sura yote kama novel tu.


Naamini you will get something to meditate about. Njaa,umasikini na ugumu wa maisha unaenda soon kuwafikisha wananchi kuamua kama hawa Wakoma.Lakini wema unaweza kuushinda ubaya kama hekima ni msingi wa fikra.


" Waaramu Wakimbia"


3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?.


4Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.


Hofu ni njia anayotumia shetani kutenda miujiza.Miujiza ya shetani huwa ni mateso na mauti.Mnaogopa watu wa Ngorongoro kuambiwa nini kama sababu yenu ya kuwahamisha kwa nguvu ni sababu muhimu ? Angalieni msiendelee kupungukiwa busara kwa kiasi hiki kwani mnaipeleka Nchi kubaya sana.


Kuongea kuna cool hasira lakini kuzuia watu kuongea kunakatisha tamaa na kufedhehesha nafsi.


Nafsi ikichoka maisha yanapoteza thamani sana na maisha yakipoteza thamani binadamu anaweza kufanya chochote.


Msiwatazame Wamasai ktk mavazi yao ya asili kama watu wanyonge na washamba ,mtakuwa mnakosea sana.Machafuko ya Nchi njia yake ni nafsi nyingi zinazoenelea kuumizwa na kukata tamaa.


Nawaonya na kuwashauri ni muhimu sana mkaanza kupuuza mkakati wenu wakutumia nguvu haswa kipindi hiki ambacho maisha ya watu yanaendelea kuwa magumu sana.


Kuna siku mtaamka na kusema hivi kweli hawa ni wale watu tuliokuwa tunawafanya tunavyotaka?.


Mna hatarisha usalama wa Nchi yetu kwa sababu ya kufikiri usalama wa Nchi unatokana na nguvu ya dola na sio busara ya uongozi.Tunahitaji kibali cha utalii kwenda kuongea na wananchi?". 

Comments