NAIBU WAZIRI KIKWETE ATOA MIFUKO 200 YA SARUJI ILI KUJENGA MADARASA MANNE YA SHULE YA SEKONDARI YA RIDHIWANI KIKWETE.

UWEKEZAJI KATIKA ELIMU NA AFYA NDIYO UKOMBOZI WA WATANZANIA-KIKWETE.

NA LUCAS MYOVELA _ KIWANGWA, CHALINZE.


Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora, Ndg. Ridhiwani Kikwete amefanya ziara katika Kata ya Kiwangwa ambapo ameongea na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Kijiji hicho hususani katika swala zima la maendeleo katika eneo hilo. 

Katika kikao hicho Mbunge wa Chalinze Ndg. Kikwete alitumia fursa hiyo kukabidhi mifuko 200 ya seruji kwa uongozi wa serikali ya kijiji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari ya Ridhiwani Kikwete inayojengwa katika Kijiji cha Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa. 


Akizungumza katika kikao hicho, Kikwete aliwashukuru wadau mbalimbali wanaochangia maendeleo katika halmashauri hiyo na kuwahimiza wadau wengine wanaoguswa kuchangia shughuli mbalimbali na si kusubiri serikali.

"Niwaombe viongozi wenzangu kuhakikisha mnasimamia ujenzi na thamani ya michango inayotelewa ionekane kwa faida ya jamii tunayoiongoza na kuleta jita na mafanikio katika taifa". Alisema Kikwete.


Akizungumza baada ya kupokea mifuko hiyo ya Seruji, Diwani wa kata hiyo Ndg. Malota Kwaga amemshukuru Mbunge na kuwaomba viongozi wenzake kuendelea kumuunga mkono Mbunge kwa kazi nzuri anazozifanya akishirikiana na uongozi mzuri wa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan. 


Aidha Ndg, Kwanga, aliwakumbusha viongozi wengine pamoja na wananchi juu ya juhudi mbalimbali anazofanya Mhe. Rais kwa ajili ya watu wa Kiwangwa na Chalinze ni za kipekee huku akishukutu serikali kwa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 2 zilizopelekwa katika kata hiyo kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo zahanati, shule ya sekondari, umeme, maji n.k.

Aidha pia Naibu Waziri Kikwete altembelea zahanati ya Kiwangwa ambayo inapangwa kupanuliwa kuwa kituo cha Afya ili kuhudumia wananchi wa kata hiyo kwa wingi zaidi.


Akizungumza Mbele ya Naibu Waziri Kikwete, Diwani Malota alimwambia Ndg. Mbunge kuwa, zahanati hiyo inapokea wagonjwa zaidi ya 3000 kwa wiki hivyo kuwa moja ya zahanati zinazo hudumia watu wengi ukizingatia kuwa shughuli za kilimo zinafanyika sana katika eneo hilo.


Comments