MAFANIKIO MAKUBWA YA ELIMU YAONEKANA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.

PATO LA NDANI BILIONI 26 CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.

 Na Lucas Myovela _ Arusha.

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Kimejinadi kwa kufikia mafanikio makubwa ya elimu hapa nchini kutokana na ongezeko la mitaala mbali mbali ya Elimu na kufanya pato la ndani kufikia kiasi cha shilingi Bilioni 26 sawa na ongezeko la shilingi Bilioni 15 kutoka mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa chuo hicho Prof, Eliamani Sedoyeka, wakati alipokuwa akizindua ripoti ya chuo hicho, Amesema mafanikio hayo ni pamoja na kujengwa Kituo kikubwa cha kisasa cha Habari na mawasiliano kwa nchi za Afrika ( ICT ) ambacho kitaanza kufanyakazi mwaka 2024.


Aidha ameeleza mafanikio mengine yametokana na ongezeko la wanafunzi wanao jiunga na chuo hicho katika masomo kukua na kufikia wanafunzi elfu kumi na tatu (13,716) huku lengo kuu ni kufikisha wanafunzi elfu kumi na sita (16,000) chuoni hapo.

"Tumefikia mafanikio makubwa kiasi ambacho sisi kama chuo tunaona tumepiga hatua kubwa sana katika kukueza elimu yetu haoa nchini kitu ambacho kimetusukuma kujenga matawi ya chuo chetu (Campus) katika maeneo mbali mbali ikiwemo Dodoma, Babati, Songea. Pia tuendelea na Ujenzi wa tawi la Ruvuma, kusomesha Wahadhiri,na watumishi wa kada mbalimbali". Amesema Prof, Sedoyeka.


"Pia Wanachuo wetu wanapata mafunzo ya Uhasibu na mafunzo ya mbinu za kisasa za Ulinzi wa nchi kupitia mtandao, (Cyber security) kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi wenye digrii yanatolewa kupitia chuo cha Polisi Moshi (CCP), Pia katika mafanikio haya tunasomesha Wahadhiri ngazi ya Uzamivu (PHD,52), mastars 9, digree ya kwanza 4, na watumishi wa kada zingine ili wafikie kiwango Cha digree. Lengo ni watumishi wote wafikie madaraja ya juu ya Elimu". Aliongeza Prof, Sedoyeka. 

"Tutaendekea kutoa Shahada ya Usalama wa kimtandao na Shahada uzamili katika fani ya mkakati wa mafunzo ya ulinzi (strategy study) na Shahada ya pili ya Usalama (Peace Security)". Ameongeza Prof, Sedoyeka.


Pia Prof, Sedoyeka ameeleza kwamba chuo hicho kinaendeleza mahusiano mazuri na Jeshi la wananchi JWTZ pamoja na Jeshi la Polisi lengo kuu ikiwa ni kuwezesha Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kupata mafunzo mbalimbali chuoni hapo kwa mafanikio endelevu kwa Taifa. 

"Mafanikio mengine ni kuboresha mitaala ya masomo ili iendane na wakati na tayari mitaala 30 ipo kwenye maboresho ambayo hufanyika Kila baada ya miaka mitano. Pia lengo la chuo chetu Katika kipindi cha miaka kati ya mitatu hadi minne ni kuwa na Wahadhiri wenye PHD kati ya 30 hadi 40 ili kuongeza ufanisi wa kitendaji na utoaji katika utoaji elimu bora kwa wanachuo wetu". Ameeza Prof, Sedoyeka.


Aidha katika hatua nyingene Prof, Sofoyeka ameelezea maendeo ya Ujenzi wa majengo na matawi ya chuo hicho yanayotekelezwa kwa fedha za ndani kupitia force account na pia benki ya Dunia imetoa mkopo wa Dola milioni 21fedha ambazo zinawezesha chuo na matawi yake kuboresha miundo mbinu ikiwemo Ujenzi wa Kituo cha Habari na mawasiliano Kwa nchi za afrika pamoja na Ujenzi wa hosteli za kisasa.


PICHA ZA UJENZI UNAO ENDELEA KATIKA BAADHI CUMPUS ZA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.

DODOMA.



HOSTEL PAMOJA NA MAJENGO YA UTAWALA KATIKA CAMPUS YA BABATI MKOANI MANYARA. 






PGD BUILDING & HOSTEL MAIN CAMPUS ARUSHA.

Comments