WASHIRIKIANA NA WALINZI KUTOKA KAMPUNI YA WENGWE SECURITY.
CCTV CAMERA YAONYESHA WALIVYO INGIA NA KUTOKA.
KITITA CHA MILIONI MBILI KITATOLEWA KWA ATAKAE BAINI WALIPO.
Mwandishi wetu _ ARUSHA.
Arusha. Majambazi wakiwa na silaha za jadi na za moto wamevamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Predators Safari Club naArusha Water Drilling,Yusuph Khan na kujeruhi kisha kupora fedha taslimu shilingi milioni 30 pamoja na dhahabu vyenye thamani ya shilingi milioni 15.
Majambazi ambao hao ambao walikuwa zaidi ya saba kwa kushilikiana na walinzi wa kampuni ya wengwe security waliyo kuwa lindo siku hiyo ya tukio wamenaswa na CCTV Camera zilizo zunguka nyumba hiyo ambapo walifunguliwa Geti na walinzi hao na kisha kuanza kazi ya upekuzi ambapo pia kuna karakana ya Kampuni hiyo kubwa ya Utalii.
Wizi huo umetokea Septemba 10, saa 2 usiku katika eneo laKiranyi Sakina, wilayani Arumeru, baada ya majambazi hayo, kumvamia Mkurugenzi huyo, wakati akiingia nyumbani kwake.
Khan ameeleza kwamba majambazi hao, kabla ya kufanya wizi huo wa kikatili walifunguliwa mlango wa kuingia ndani na walinzi wa kampuni binafsi ya Mwengwe ambao nao baada ya tukio hilo walikimbia na majambazi hao baada kutimiza hadhima yao.
"Nilikuwa na familia yangu naingia ndani na ndipo nilivamiwa na majambazi ambao mikononi walikuwa wameahika silaha mbali mbali na kunijeruhi kisha kuingia ndani na kuchukuwa fedha na vito vya thamani baada ya kuwaweka chini ya ulinzi familia yangu "alisema.
Alisema baada ya tukio hilo, walinzi waliokuwa zamu,Moses Alfred Mabula (46) na Lazaro Richard Pruza(37) wote wakazi wa eneo la Daraja mbili jijini Arusha walikimbia na kuondoka na majambazi hao.
"Kamera za usalama zinaonesha walinzi ndio waliwafungulia mlango majambazi na kuingia ndani kupora na baada ya hapo wamekimbia na hawajulikani walipo"alisema
Khan aliomba Jeshi la Polisi na Serikali kusaidia kukamatwa walinzi na majambazi hao, kwani fedha zilizoporwa alikuwa amepokea jumamosi jioni baada ya kuuza gari aina ya Mitsubishi Canter yenye namba za usajili T196 DRX .
"Baada ya tukio tulitoa taarifa polisi ambao walifika na kuanza uchunguzi na tayari kesi imefunguliwa"alisema
Meneja wa kampuni ya predators Safaris Club Ltd , Stive laizer alisema kampuni hiyo, itatoa zawadi ya shilingi milioni 2 kwa ambao atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na walinzi hao.
"Hili ni tukio la kupangwa sasa ambao atawezesha kukamatwa na polisi walinzi waliotoweka tutatoa zawadi ya shilingi milioni mbili"alisema
Kamanda wa polisi Mkoa Arusha Justine Masejo amekiri kutokea kwa tukio hilo la ujambazi na kueleza kwamba uchunguzi umeanza ili kubaini kiini cha tukio hilo.
Meneja wa Kampuni ya Ulinzi Wengwe Security Juma Masuka amesema wanawatafuta walinzi wao baada ya kuhusika na wizi huo.
"Wameoneoana kwenye CCTV wamewafungulia mlango majambazi na baada ya kuiba wamekimbia na wao na tunawasaka"alisema.
MWISHO
Comments
Post a Comment