PROF, MKENDA WAKAGUZI WA NDANI SIMAMIENI IPASAVYO MATUMIZI YA FEDHA KWA MAENDELEO YA TAIFA.

WAZIRI CHANDE AWATAKA KILA MMOJA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE IPASAVYO.

Na Lucas Myovela _ Arusha.


ARUSHA: Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof, Adolph Mkenda amewataka wakaguzi wa ndani kudhibiti na kusimami ipasavyo matumizi ya fedha za serikali ili taifa liweze kupiga hatua kubwa kwa maendeleo ya wananchi.

Prof, Mkenda ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 16 wa wakaguzi wa ndani wa Bodi na Taasisi unaofanyika katika ukimbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.


Prof, Mkenda ammeeleza kuwa Wakaguzi wa ndani ni watu muhimu kwa ustawi wa taifa na kwakupitia maafisa masuhuli kufanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa na wakiweza kudhibiti ipasavyo matumizi ya fedha za serikali ni dhahili watanzania wengi watanufaika kwa maendeleo yanayo pangwa na kutekelezwa na Serikali.

" Kipindi nikiwa Afisa masuhuli niliona umuhimu Mkubwa sana wakuwatumia Wakaguzi wa ndani nia ilikuwa ni kuweza kujua sehemu gani inaleta tatizo na niliweza kuweka sawa kwa sababu suala Kubwa ni kujenga sio kusubiri ubadhirifu au upotevu wa Mali ya umma utokee ndio hatua ichukuliwe hatua mara nyingi tudhibiti haraka kuliko kusubilia matatizo". Amesema Prof, Mkenda.


"Wakaguzi wa ndani wakitumika ipasavyo na wakijitoa kwa aajili ya serikali itasaidia kuchukuwa hatua za haraka kabla ya upotevu wa fedha za miradi na itakuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa jamii na Serikali itafanikisha malengo yake kwa Jamii". Aliongeza Prof, Mkenda.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na mipango Mhe, Hamad Chande, Amewataka Wakaguzi wa ndani kutokubali kuachwa nyuma katika utendaji na ufanisi mkubwa wa kazi na badala yake kuchukuwa hatua haraka za Ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya fedha za umma pamoja na kuelekeza nini cha kufanya kabla ya madhara kujitokeza.


Mhe, Chande ameeleza kuwa zoezi la mchakato wa Taasisi za umma na binafsi lazima wawashirikishe wakaguzi wa ndani ili kuleta matokeo chanya na ya haraka ili kuokoa fedha za umma iwapo watashirikishwa kuanzia mwanzo wa mchakato wa jambo husika.

"Sisi kama wizara ya Fedha ambao ndiyo tunadhamana ya kuwasimamia na kuwaeleza, Tumejadiliana mengi ni imani yangu kwa kila mmoja akifanya kwa ufanisi kutokana na nafasi yake basi taifa letu litapiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya ujenzi wa Tanzania". Amesema Chande.


"Mhe, Rais wetu Dkt, Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta fedha za maendeleo ili tuweze kupiga hatua, Sasa basi hizi fedha tukiweza kuzisimamia ipasavyo zitakuwa na mafanikio makubwa sana kwa wananchi wetu na dhamira ya Mhe, Rais ikawa imetimia kwa kiasi kikubwa kama siyo kumaliza changamoto za wananchi". Alisisitiza Mhe, Chande.


"Miradi imayo inayo anzishwa na kuendelezwa Serikali inaweka fedha nyingi sana katika miradi hiyo inahitaji usimamizi wa karibu na wakutosha ili kuondoa dosari zozote za kutokamilika kwake na nyie ndiyo wenye jukumu hilo sasa basi haina haja ya kusubilia kusongamana ndiyo mtimize wajibu wenu". Alisistiza Chande.


Awali Rais wa Umoja wa Taasisi ya Wakaguzi wa ndani Tanzania IIA CPA, Zelia Njeza, amesema Hadi Sasa Tanzania haijafanya vizuri katika upande wa uanachama na kutoa wito kwa Wakaguzi wote wanaofanya Kazi za Ukaguzi wa Ndani waweze kujinga na Taasisi hiyo ya IIA.


"Mbali na ugumu wa kazi zetu nado pia tunakutana na vitisho mbali mbali wakati wa kutimiza majuku yetu, Niwaombe na niwasihii wadhibiti wenzangu tusife moyo tuendelea kulitumikia taifa letu kwa maslahi ya taifa letu". Amesema Njeza.


Njeza Ameeleza kuwa moja wapo ya Maslahi mapana ya kuwa mwanachama ni pamoja kusaidiwa pale unapokuwa na changamoto ya kikazi pamoja na kupata hati ya kitaifa na kimataifa ya kutambuliwa pia inakundaa vyema katika utendaji wa Kazi kwa Wakaguzi wasiyo wahasibu wanaweza kupata misingi ya Taaluma nzima.






Comments