MKUU WA MKOA WA MANYARA APONGEZA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MATI SUPER BRANDS LIMITED
Na Mwandishi wetu_ Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amepongeza uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji vikali cha Mati Super Brands Limited kilichopo Wilayani Babati Mkoani Manyara, ambacho kimekua mstari wa mbele katika ulipaji kodi kwa serikali pamoja na kujitoa kusaidia jamii inayowazunguka kiwanda hicho kwa kutoa misaada mbali mbali.
Akizungumza mara baada ya kutembea kiwanda cha hicho cha Mati Super Brands Limited,Mkuu wa Mkoa wa Manyara amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa ubunifu na umahili wa kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana wa Mkoa wa Manyara.
"Sisi kama serikali tunawapongeza kwa ulipaji mzuri wa kodi za serikali ambayo inachangia Maendeleo kwa taifa kwa ujumla, Pia mmekua mstari wa mbele kujitolea katika masuala ya kijamii huu ndiyo uwekezani wenye tija kwa taiga hasa pale mnapoisaidia serikali kusaidia wananchi wake kwa huduma mbali mbali na huo ndiyo uzalendo wa kweli". Amesema Sendiga.
Aidha Sendiga amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na yenye tija kwa wawekezaji ili waweze kufanya kazi zao bila usumbufu wowote kibiashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited David Mulokozi amepongeza serikali ya Awamu ya Sita ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora kwa wawekezaji na wafanyabiashara.
"Kwa sasa tunayo serikali ambayo imeweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi inatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya kazi na kulipa kodi kwa kwa wakati kwa kumjali muwekezani kutokanaa na mazingira ya kibiashara ilivyo". Anaeleza Mulokozi
Comments
Post a Comment