SERIKALI INATOA PESA NA KAZI ZINAFANYIKA WATU WAACHE MAJUNGU NA UPOTOSHAJI

VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI YA SERIKALI IPASAVYO ILI KUENDANA NA THAMANI YA PESA.


SEKTA YA ELIMU NA AFYA INAZIDI KUKUA ZAIDI LENGO NI WANANCHI WAPATE HUDUMA STAHIKI KAMA ILIVYO AHADI YA RAIS SAMIA.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Viongozi wa chama na Serikali wametakiwa kuisemea Serikali kwa mambo mazuri mbali mbali ya maendeleo inayo yafanya ambayo ni mazuri kwa wananchi na kuleta maendeleo yenye tija kwa jamii, Pia kushauri na kutoa mawazo chanya ili kuresha huduma kwa jamii kuliko kubaki kuchambua mabaya ambayo hayana ukweli wowote.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Mjini Ndg, Timoth Sanga, wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbali mbali ya Elimu na Afya inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.


Kisanga amesema kuwa CCM ilipokuwa inaomba lidhaa ya kuongoza nchi hii mwaka 2020 iliweka vipaumbele vyake ambavyo itavitekeleza katika kipindi cha miaka mitano ambapo miongoni mwa vipaumbele hivyo vikiwemo Elimu na Afya.

"Tuliona katika Sekta ya Elimu ni bora kuikuza elimu yetu hapa nchini ili kuzidi kukuza vijana wetu na kuwa na taifa lenye wasomi wengi na wataalamu ambao watatusaidia kukuza taifa letu katika nyanja mbali mbali na Serikali imeamua kulitimiza hilo nimpongeze Rais wetu Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika sekta ya elimu ili kutimiza malengo ya ilani ya chama kwa wananchi". Alisema Sanga.


"Na sisi kama viongozi tunaendelea kutoa ushawishi aendekee hivi na kwa wake wasaidizi wake wasivunjike moyo kwa maneno machache ya mitaani kikubwa wasimamie maendelei sisi kama chama Wilaya tutaendelea kuwapambania ili maendeleo ya wananchi wetu yafanikiwe maana kama pesa za maendekeo zinatolewa hatuwezi kwamishwa kwa maneno ya upotoshaji". Aliongeza Sanga.

Aidha Kisanga aliwataka watumishi wote na viongozi kuendekea kuwa waaminifu pindi wanapotekeleza miradi mbali mbali ili kulinda heshima na kuifanya thani ya fedha kuonekana katika miradi hiyo ambayo ni msaada mkubwa kwa jamii yote ya watanzania

"Fedha hizi ni zawatanzania ambao wamejibana kwa matumizi yao na kulijenga taifa lao, niwaombe sana viongozi na wasimamizi kuwa waamifu ili kutimiza miradi hii kwa wakati na inapo timizwa ionekane thamani ya fedha kwenye kila mradi husika ili nchi ikaimarike na niwaombe watanzania wenzangu kulinda rasilimali hizi ili zidumu kwa maendeleo ya vizazi vyetu". Alisema Sanga.

Pia kisanga aliwataka wazazi wote kuto wazuia vijana wao kupata elimu maana kwasasa mazingira ya upatikanaji wa elimu ni bora zaidi na serikali inaendelea kutoa elimu bure na kuboresha miundombinu ya elimu hasa kwa kuweka mabweni ili wanafunzi wasitembee umbali mrefu.


Aidha pia alitoa wito kwa wakina mama kuacha tabia ya kujifungulia nyumbani na kufanya watoto kutopata huduma bora za Afya ilihali tayari Serikali imeshaweka vituo bora vya Afya kwaajili ya mama na mtoto.

Kwa upande wake Naibu Meya wa Jiji la Arusha Ndg, Abraham Mollel, Ameeleza kuwa wao kama Jiji la Arusha wamejipanga vyema kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na Serikali inakamilika kwa wakati na inatoa huduma kwa wananchi na kuweka wataalamu wa kutosha kuhakishasha huduma bora zinapatikana kwa wananchi.

"Tunaendelea kusimamia ipasavyo miradi mbali mbali inayoendelea kutekelezwa na serikali hasa katika sekta ya elimu tuaweka mabweni ya kutosha ili kuwasaidia wanafunzi wetu wasitembee umbali mrefu na kuweka miundo mbinu mingine mizuri ya kujisomea lengo letu ni tuwe na wasomi kwa maendeleo ya nchi". Alisema Mollel.


"Katika Sekta ya Afya tunaendelea kuweka vifaaa vya kisasa na watalamu zaidi ili kutoa huduma bora kwa wanchi wetu pa kuboresha makazi ya watumishi wetu pamoja na maslahi yao nimshukuru sana Rais Samia kwa kutoa fedha hizi za maendeleo ambapo zinaenda kutoa huduma kwa kila mtanzania". Aliongeza Mollel.

Awali wakitoa taarifa za miradi hiyo ya ujenzi, wakuu wa shule za Sekondari ya Korona pamoja na Mrisho gambo walipongeza uongozi wa halmashauri ya Jiji la Arusha kuendelea kutoa fedha mbali mbali ili kukamilisha miradi hiyo na kuifanya kuwa chachu ya maendeleo makubwa ya ukuaji wa elimu hapa nchini.

"Tulipokea kiasi cha shilingi milioni 828 na laki 6 mwezi may 2023 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 11, matundu 16 ya vyoo pamoja na mabweni 14, ambapo ujenzi huo tulianza mapema mwezi Juni 2023, ambapo mpaka sasa mwezi huu wa septemba 2023 ujenzi wote umefikia 99% ili kukamilika". Amesema Christopha Malamsha Mkuu wa Shule ya Korona Sekondari.

"Pia kwa mwezi huu tumepokea milioni 130 kwaajili ya ujenzi wa bweni ambapo fedha hiyo niya Mradi wa EP4R na tayari tumesha anza ujenzi huo, Pia kupitia halmashauri yetu Mkurugenzi ametupatia milioni 50 kwaajili ya kuweka tyliz pamoja na ununuzi wa vitanda na vyote tumesha vifanya tumamshukuru sana maana fedha hizi hatukuwa nazo na pia amekea taa za kutosha wanafunzi kujisomea usiku". Aliongeza Malamsha.

"Mradi huu tunaoutekeleza unagharimu shilingi milioni 138.7, ambapo ni fedha za TASAF pamoja na fedha zitokanzao na mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha ambazo ni shilingi milioni 12.73, kwa utoaji wa fedha hizi zitaweza kukamilisha ujenzi wa bweni pamoja na bwalo la wanafunzi na utaongeza ufanisi na usalama zaidi kwa wanafunzi maana watakuwa mazingira ya shule kipindi chote cha masomo". Alisema Mwalimu Aman Maligana Kaimu Mkuu wa Shule ya Mrisho Gambo Sekondari.

Kwa upande wake katibu wa vijanawa ccm ( UVCCM ) wilaya ya Arusha Mjini Ndg, Mohamed Massud Mohamed, Amesema kwasasa siyo muda wa kusikiliza majungu na maneno ni wakati wa kufanya kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kama inavyo hitaji ipanai ya CCM na kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan.


"Sisi kama vijana tuliyopata nafasi ya kuaminiwa na Mhe, Rais tunapaswa kuhakikisha yale yote serikali inayofanya tuyasimamie kwa ukaribu na kushauri ili tusonge mbele kama taifa moja,maana lengo la Mhe, Rais ni kuhakikisha taifa linapata maendeleo". Alisema Mohamed.

Aidha pia Mohamed aliweza kuwashauri wanafunzi wazingatie elimu maana ndiyo mkombozi wa maisha yao na taifa kwa ujumla na kuwakanya vijana waliyopo mtaana wanao warubuni wasichana waliyopo masomoni na kuwahaidi kuwa serikali haita wafumbia macho kamwe endapo watakapo bainika kutenda makosa hayo.

























Comments