KAMPUNI YA TIGO KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUKUZA SEKTA YA UTALII KWA KUTOA HUDUMA BORA YA KIMTANDAO.
Na Lucas Myovela _ Arusha.
Kampuni ya Mitandao ya Simu Hapa nchini ya Tigo imesema itaendelea kuboresha mawasiliano na kuifikia jamii yote kwa utoaji huduma bora kwa wananchi hasa kwapindi hichi ambapo mapinduzi ya kimtandao yanahitajika katika kukuza uchumi wa taifa.
Akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha meneja wa kampuni ya Tigo Kanda ya Arusha Ndg, Daniel Meinoya mara baada ya ufunguzi wa Tamasha la Maasai Festival linalo endelea kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro Jiji Arusha.
Meinoya amesema Kampuni ya Tigo itaendelea kusaidia jitihada za Serikali katika kukuza utalii kupitia matamasha mbalimbali ya kitamaduni ili kuchochea uchumi wa taifa kupitia huduma zake za mawasiliano zilizoenea kote nchini hasa katika utoaji wa huduma ya kulipa kidigitali kwa kumia tigo maana itamsaidia mgeni kufanya miamala yake kwa wepesi.
"Tigo inatambua umuhimu wa tamasha hili ambalo lengo lake ni kuzijua tamaduni zetu za asili na hatuwezi kubaki nyuma lazima tuwe sehemu ya kuchochea utalii wetu kama chanzo cha mapato ya taifa leo hasa kwa kurahishisha huduma za kimtandao kwa watanzania na sehemu zote zenye vichocheo vya utalii hapa nchini". Alisema Meinoya.
"Tanzania ndiyo nchi pekee inasifika kwa vivutio mbali mbali na adhimu duniani wageni wanapokuja kutalii hapa nchini wanatumia huduma za Internet kwa ajili ya mawasiliano na sisi Tigo tupo hapa kuhakikisha Tunawawezesha wageni wetu wanapata huduma bora za kimtandao ilikuendelea kufanya mawasiliano mbali mbali na huduma mbali mbali kadri ya mahitaji yao". Aliongeza Meinoya.
"Na sisi kama tigo tumejipanga hasa kwa siku hizi tatu katika viwanja vya Ngarenaro kuwaletea huduma zetu ambazo zinaweza kusaidia katika kukuza mawasiliano na wateja wakitembelea tamasha hili watakutana na huduma zetu na ninaamini watazifurahia huduma bora kutoka kwetu". Alisisitiza Meinoya.
Aidha Meinoya alieleza kwamba wataendelea kuunga Juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kukuza Utalii wa Utamaduni pamoja na Utalii nchini Kwa kuendelea kudhamini matamasha mbali mbali ambayo yanaleko la kutangaza taifa la Tanzania kwa namna yeyote.
Akifungua Tamasha hilo la siku tatu la Maasai Festval katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha Ndg, David Lyamongi amewataka viongozi wa kimila na Machifu wanao aminika na jamii kuendelea kudumisha misingi ya Mila pamoja na kutunza amani, mshikamano na Umoja wa Watanzania maana ndiyo tunu ya Taifa.
Lyamongi amesema Tamasha hilo la Wamaasai ni nguzo muhimu ya kuendeleza mshikamano na Umoja kupitia tamaduni zao ambapo ndani yake kunachochea na kukuza utalii pamoja na Utamaduni nchini ili kuvutia wageni.
“Niwaombe viongozi wetu wa Mila zetu kujenga misingi ya Maendeleo ya tamaduni zetu ili kuendelea kuvutia utalii wetu kwa kuziendeleza tamaduni zetu baada ya wageni kutembelea vivutio vyetu wapate muda wa kuendelea kuwepo nchini na hivyo kuongeza mapato yetu na taifa”. Amesema Lyamongi.
"Rais wetu anaendelea kupambana kutangaza utalii wetu ni jukumu letu sisi kumuunga mkono ili tuweze kulikuza taifa kwa pamoja niwapongeze wote waliyo shiriki hasa wale wote waliyo dhamni Tamasha hili adhimu kufanyika kwa uzuri na ubora ni imani yangu kila mmoja wetu akifanya majukuyake tutapiga hatua kwa pamoja kama Taifa". Aliongeza Lyamongi.
Nae Mkurugenzi wa Tamasha hilo la Maasai Festival Saitabau Nkemwa alisema Tamasha hilo lilianzishwa Kwa lengo la kutangaza Utalii wa kiutamaduni.
Alisema wameanza na kabila la Wamaasai Kwa Sababu ndilo kabila pekee lililodumu kwenye Tamaduni zake hadi Leo sanjari na kuunga Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan baada ya filamu ya Royal Tour kufungua utalii nchini.
Tamasha hilo linalo endelea Jijini Arusha kwa siku tatu ambapo linahudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, Wageni kutoka kila kona ya ulimwengu na makampuni binafsi huku Kampuni ya TIGO ikiwa ni Mmoja ya wadhamini wa Tamasha hilo.
Comments
Post a Comment