WAZIRI KIKWETE AWATAKA WATUMISHI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WANANCHI HARAKA KABLA YA KUFIKA KWA VIONGOZI WA KITAIFA.

SHUGHULIKIENI MALALAMIKO YA WATEJA KWA WAKATI. KIKWETE

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi kutoka taasisi zote za Serikali ma Umma kutatua malalamiko na changamoto za wananchi kwa wakayi ili kuondoa msongamano wa wananchi katika ofisi za juu zaidi.

Ameyasema hayo wakati wa kufunga Kikao Kazi cha Taasisi Simamizi za Madili katika Utendaji, Kitaaluma na Watumishi wa Umma kutoka Wizara na Taasisi za Umma katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma.


Kikwete ameeleza kwamba nimatarajio ya Serikali kila mtumishi wa umma akiwanibika ipasavyo katika majukumu yake atasaidia wananchi wengi kupata huduma kwa wakati na itaonfoa lawama kwa viongozi kila siku kulalamikiwa.

"Nimatarajio yangu kuwa ninyi kama wawakilishi wa watumishi katika Taasisi zenu, mtakuwa chachu kwa wengine katika uzingatiaji wa maadili, hakikisheni mnatatua malalamiko ya Wananchi ili kuwapunguzia viongozi wa kitaifa kutatua malalamiko ambayo yangeweza kutatuliwa katika sehemu zanu za kazi." alisema Kikwete.


"Maadili mema ni msingi mkubwa katika utoaji haki, hivyo Watumishi wa Umma zingatieni maadili ili haki itendeke wakati wote wa utoji huduma kwa wanachi wetu pasipo upendelevu au ushawishi wa jambo fulani". aliongeza Kikwete.

Aidha Naibu Waziti Kikwete aliwakumbusha washiriki hao kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi katika sehemu zao za kazi na zaidi kuwa kiungo kizuri kati ya Serikali na Wananchi katika utoaji huduma bora.

Comments