WAZIRI KIKWETE: HATUTOKUWA NA HURUMA NA WANAOWAONEA WANYONGE.

 AWAONDOA WARATIBU WA TASAF WA MKOA NA WILAYA WALIYOSHINDWA KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI.

Na Ofisi ya Naibu Waziri.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora amewataka watumishi hapa nchini kufanya majukumu yao kwa wananchi ma kueleza kuwa Serikali haito kuwa na huruma kwa mtumishi yeyote ambaye hawajibiki kwa wananchi.


  Kikwete ameyasema hayo  Mkoani Mara wakati waziara yake ya kikazi ya kutembelea na kuongea na Watumishi katika Manispaa ya Musoma na kisha kufanya ziara kukagua utekelezaji wa mpango wa kuondoa Umaskini yaani TASAF katika wilaya hiyo.


Kikwete  ameeleza kwamba yeye kama Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, hatoweza kuwafumbia macho watumishi wote wanakwenda kinyume na mlengo wa serikali wa kusidia wananchi ili kujikwamua kiuchumi kutokana  na pesa ambayo serikali imekuwa ikizitoa kwa wananchi.

Pia katika tukio jengine,Naibu waziri Ndg. Kikwete amewaondoa kwenye Uratibu wa mpango wa TASAF waratibu wa Mkoa na Wale wa Wilaya kwa kile alichokiita kushindwa kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wangonge ambao wanahitaji sana huduma hii katika muda. Akionyesha kukaairishwa na kushindwa kwao , Ndg. Kikwete alimuelza RAS wa Mkoa wa Mara ndugu Makungu kutoelewa kwa nini hadi leo wahitaji hao hawajalipwa wakati Fedha kwa ajili ya wanufaika zilishatumwa wakalipwe wanufaika. Naibu Waziri anaendelea na ziara Mkoani hapo kwa kuelekea Wilayani Tarime.


Naibu Waziri ambaye ana ziara ya siku tatu katika Mkoa huo alikuwaelekeza Watumishi wa Umma kujikita katika kuhakikisha wanazingatia na kutafsiri maono ya Rais Samia Suluhu Hassan pale aliwahimiza kuwe na Utumishi wenye kuleta tija, mbora, ulio kimkakati unaolenga kuwatumikia Wateja ambao ni wananchi. Akizungumza na watumishi, Ndg. Naibu Waziri aliwaasa kuwa wabunifu na wenye mikakati ili kufikia malengo.







Comments