🔴BREAKING NEWS : MAFUTA YAPANDA BEI USIKU WA MANANE, RAIS SAMIA AKIWA DOHA.

⛽️:Mafuta Yapanda Bei nchini,Bei Mpya Kuanza Leo Jumatano October 04, 2023 saa 6:01 usiku 


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia leo Jumatano October 04, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi October 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3281 kwa lita, dizeli Tsh. 3448 na mafuta ya taa 2943.


EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi October 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa kufikia 4.21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi kufikia 17% kwa petroli , 62% kwa dizeli na 4% kwa mafuta ya taa, pia uamuzi wa Wazalishji wakubwa wa mafuta Duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo Urusi imewekewa na Mataifa ya Magharibi.

📄:Ewura Mkeka.




Comments