DKT BITEKO - UONGOZI MZURI NI ULE UNAOBADILISHA MAISHA YA WATU.

 AWATAKA WANASIASA KUFANYA SIASA ZENYE KUJIBU CHANGAMOTO ZA WANANCHI.

Na Lucas Myovela,Chalinze.


NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt, Dotto Biteko amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kufanya siasa za kubadilisha maisha ya watanzania ili kuwaletea maendeleo badala ya kufanya siasa za maneno matupu zisizojibu hoja na kuleta mabadiliko yeyote kwenye jamii.

Dkt, Bitekoameyasema hayo wakati wa mkutano maalum wa jimbo la Chalinze wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2023, Mkutano uliyo udhuliwana wanachma wa chama hicho akiwemo Rais Msfafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja Mbunge wa Jimbo hilo la Chalinze Mhe, Ridhiwani Kikwete.


Dkt, Biteko ameeleza kuwa kwa sasa ni wakati kwa wanasiasa hasa wa CCM kujibu kwa hoja kutokana na mafanikio makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassani ambaye kupitia ilani ya chama cha mapinduzi kwa mwaka 2020-2025 inatekelezwa ipasazyo na wananchi wanaona jinsi serikali inavyo waangaikia ili kukomboa uchumi wa taifa.

"Niwahase sana watumishi wa Umma kuwahudumia wananchi na kuwafuata walipo pasipo kuwasubiria walete kero zao kwenye madawati, maofisini au kusubilia viongozi wanapo fanya ziara ndipo watatue kero za wananchi ili hali nyie mpo mnalipwa mishahara na serikali ili kuwahudumia wananchi". Alisema Dkt, Biteko.


"Nimeridhishwa na namna halmashauri ya wilaya ya Chalinze inavyosimamia fedha za miradi ya wananchi ambazo zimekuwa zikitolewa kwakweli unaona thamani ye fedha hizo na nia ya serikali ni kutaka kuona wananchi wake wanapata huduma bora na stahiki kila nyanja kuanzia, Afya, Elimu, n.k". Aliongeza Dkt Biteko.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya, aliweza kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Dkt, Dkt Mashaka Biteko kuwa naibu waziri Mkuu wa tatu toka Tanzania kupata uhuru wake na kueleza kuwa rais hajakosea katika kufanya uteuzi huo wa Dkt, Biteko.


"Uteuuzi wa Naibu Waziri Mkuu Biteko sio jambo la kushangaza kwani ni Naibu Waziri Mkuu wa tatu sasa wapo marais wengine nao walisha fanya hivyo na wala siyo jambo geni na Rais hajakeikua katiba yetu inamruhusu kufanya hivyo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya chaguo sahihi, katumia Mamlaka yake ya kikatiba". Amesema Jakaya

Akielezea utekelezaji wa ilani 2020-2023 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, anasema utekelezaji umefikia asilimia 96, na sasa hatua waliyofikia inawabeba kutembea kifua mbele kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.


Kuhusu sekta ya maji Ndg, Ridhiwani Kikwete ameeleza awali kulikuwa na asilimia 62 tu inayofikisha huduma ya maji kwa wananchi lakini sasa imefikia asilimia 96 ya upatikanaji maji kati halmshauri hiyo ya chalinze.


"Mpaka sasa tayari Bilioni sita zimeletwa katika Halmashauri yetu ya Chalinze ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali na tayari kazi imeeanza ili wananchi wetu wasipate adha yeyoyote katika upatikanajia wa huduma zote za kijamii". Amesema Ridhiwani Kikwete.


Comments