SASA WAZUNGU KUCHANJA PESA KAMA WAPO ULAYA TU.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Benki ya CRDB imeendeleza ubora wake wa kutoa huduma za kifedha hapa nchini pia katika nchi za Afrika Mashariki na sasa imeingia kimataifa zaidi ambapo imezindua Matumizi ya Kadi ya American Express ambazo zitatumika katika mashine za ATM na popote pale kutoa fedhakirahisi kwa wageni mbalimbali wanaoingia nchini Tanzania kwaajili ya shughuli mbalimbali.
Kadi hiyo maalumu ya Americans Ecpress imezinduliwa Jijini Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema ubia wa American Express na CRDB utasaidia kuchochea uchumi katika sekta ya utalii kutikana na huduma hiyo rahisi kwa wageni itakayopelekea kupata fedha kirahisi kwa kutumia kadi za America Express kutoa fedha kupitia ATM na POS za CRDB BANK .
Mongela ameeleza kuwa benki hiyo ya CRDB imekuwa kiongozi kwenye mapinduzi ya mifumo ya teknolojia ya kifedha hapa nchini inachochea ukuaji wa kiuchumi hapa nchini na kuhaidi Serikali ya Mkoa itaendelea kuunga mkono kwa kuwa benki hiyo imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo na kuzitaka taasisi zingine za fedha kuiga mfano huo wa benki ya CRDB.
"Kwa uzinduzi wa mashirikiano haya ya benki ya CRDB na American Express utasaidia zaidi kuimarisha nafasi ya CRDB kwenye maendeleo ya nchi yetu katika kuwezesha mustakabali mzuri wa mfumo wetu wa kifedha hasa katika kuinhiza fedha za kigeni kutoka kwa wageni wanaoingia hapa ncjini". Amesema Mongela.
Naye Makamu mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Profesa, Neema Mori alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza mapato na fedha za kigeni katika maeneo ya utalii hususan mkoa wa Arusha.
Alisema watalii wataweza kufanya malipo ya Serikali ikiwamo kulipia Visa na tozo nyingine stahili kwani mfumo tayari umeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa malipo ya Serikali GePG.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ,Abdulmajid Nsekela ameeleza kuwa benki ya CRDB ni benki ya kwanza ya kizalendo kuingia ubia wa pamoja na America Express ili kumrahisisha mteja yoyote duniani kutumia kadi za America Express kutoa fedha kupitia mtandao wa ATM na POS za CRDB .
"Benki yetu ya CRDB imekuwa ya kwanza kuanzisha huduma ya Tembo kadi,Viza na master kadi na kuongoza katika ubunifu,ili uweze kumfikia mteja lazima utengeneze mazingira mazuri na mepesi ya kupata huduma". Amesema Nsekela.
"Benki ya CRDB tunajivunia kwa wenzetu wa America Express kwa kuingia ubia wa pamoja kwa kuruhusu huduma hiyo ipatikane kwwnye mitandao yetu ya Pos na ATM, unapoamua na Mahusiano na America Express huyu ni mbia mkubwa sana duniani na benki yetu imetambuliwa kwa hilo". Amesema Nsekela.
Aidha Nsekela ameeleza kuwa kwa mwaka huu pekee taarifa za Fedha za benki ya CRDB zinaonyesha kuwa takribani miamala Milioni 4 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 imefanyika kupitia mfumo huu.
"Huduma ya kadi za America Express zitasaidia katika kuboresha na kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini kwani watalii wengi wanatoka katika bara la America na CRDB imekuwa ya kwanza kutoa huduma Tanapa na Ngorongoro pamoja na Zanzibar". Ameeleza Nsekela.
"Ushirikiano huu unakwenda kuleta Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi nchini mfano katika mkoa huu wa Arusha ambao ni kitovu Cha Utalii wadau kama TANAPA, Ngorongoro, TATO na wengineo wataweza kunufaika na hudumu hii Kwa urahisi zaidi na tutaendelea kuwa wabunifu Ili kuweka mazingira mazuri na mepesi Kwa wateja". Ameongeza Nsekela.
Kwa Upande wake Briana Wilsey, Makamu wa Rais, na Meneja Mkuu EMEA, Huduma za Mtandao wa Kibadilishanaji Kimataifa, American Express,alisema hadi Sasa wamefanikiwa kutoa kadi 130 katika nchi 90 duniani.
Briana alisema wameamua kushirikiana na CRDB Kwa kuwa ni benki inayokua kwa kasi ya hali ya juu,inatoa huduma nchi za maziwa makuu ambazo ni Tanzania ,Burundi na Congo,Mtandao mpana wa wadau na wananchama wake hivyo mashirikiano hayo yatataongeza mapato kupitia Sekta ya Utalii.
Comments
Post a Comment