AJINADI ARUSHA NI GENEVA YA AFRIKA LAZIMA IWE NA WATAALAMU SHINDANI DUNIANI SIO KATIKA MAJIJI.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Mapinduzi ya Miaka 5 katika Sekta ya Utalii na Urembo yaliyo fanywa na Chuo cha Volcano Jijini Arusha katika kuwakombo vijana kujiajiri na hapa Dc wa Arusha ametoa rai kwa vyuo vingine vya Utalii hapa nchini viweze kuzalisha wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa ili kukidhi soko la ushindani katika sekta ya utalii Kimataifa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe, Felician Mtahengerwa wakati alipohudhulia katika mahafali ya 5 ya ngazi ya cheti katika chuo cha utalii cha Volcano kilichopo Sakina jijini Arusha ambapo amewataka wahitimu hao kuangalia fursa za tofauti katika sekta ya utalii pamoja na ususi.
Mtahengerwa ameeleza kuwa jitihada zaidi zinahitajika kumudu ushindani katika sekta hiyo ua utalii kwa kutoa wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa, Pia amekipongeza chuo hicho kwa namna kinavyotoa elimu na ujuzi wa wanafunzi mbalimbali wanaofika chuoni hapo.
"Naomba nitoe rai kwa wahitimu kuitumia elimu mliyo ipata hapa chuoni , kwenda kufanya ubunifu wenye tija na hadhi ya kimataifa, angalieni namna ya kuanzisha na kuendesha biashara kwa kiwango cha tofauti kwa kujua watu mnao walenga ( wateja ) ili kukidhi mahitaji ya wateja wenu kibiashara". Ameeleza Mtahengerwa.
"Hivi sasa Mkoa wetu umepiga hatua sana kwenye utalii leo hii hoteli zetu zimejaa, zinahitaji wahudumu wenye weledi na viwango vya juu vya kuhudumia watalii, lakini hapa Arusha bado viwango vya wahudumu havijakaa kiushindani ila naimani kupitia chuo hiki cha Volcano kina nafasi kubwa ya kufanya mapinduzi makubwa katika sekta hii". Amesema Mtahengerwa.
"Zamani kwenye hoteli nyingi za kitalii walikuwa wameajiri zaidi wakenya lakini hivi sasa watanzania tumepiga hatua kubwa katika sekta ya utalii na mimi siwezi kubali Jiji kama Arusha lilinganishwe na jiji la Nchi jirani naami Wahitimu hawa wataenda kufanya mapinduzi makubwa". Aliongeza Mtahengerwa.
Pia Mtahengerwa alisema kuwa changamoto ndogo ndogo ni rahisi kumalizwa na vyuo iwapo vyuo hivyo vitabadili ufundishaji na kujikita kwenye ubunifu wa kimataifa ikawa ni pamoja na kufundisha Lugha za kimataifa ili kuendana na soko la ushindani duniani.
Kwa upande wake Mkuu chuo cha Volcano Ndg, Lazaro Thobias amesema chuo cha Volcano kimejikita kuzalisha wahitimu wenye viwango vya juu na wengi wa wahitimu zaidi ya asilimia 90 tayari wapo kwenye soko la ajira katika sekta mbalimbali mkoani hapa.
"Sisi chuo cha Volcano tunawaandaa vijana vizuri kwa kuwafundisha ujuzi unaoendana na teknolojia za kimaiaifa na wanaweza kufanya kazi popote duniani kwani tunawafundisha pia lugha mbalimbali za kibiashara za kimataifa". Amesema Thobias.
"Vijana wetu katika soko la ajira tumewaandaa vizuri ambapo wanaweza kutumia kompyuta hivi sasa dunia imehamia kiganjani na tehama kwa ujumla"Aliongeza Thobias.
Baadhi ya wahitimu, Charles Wambura mhitimu waongoza watalii na Rahma Dickson aliyehitimu Mapishi walisema elimu walioipata imewasaidia kuwa na uelewa wa masuala ya utalii na kukishukuru chuo hicho kwa kuwapatia elimu bora na kwa sasa tayari wanaajiriwa.
Jumla ya wahitimu waliyo hitimu katika Chuo cha Volcano ni 87 wa fani mbalimbali ikiwemo utalii,Mapishi,Ususi,Fundi Umeme na Magari walihitimu na kutunukiwa vyeti.
Hadi sasa chuo kimetoa wataalamu mbalimbali katika kila hoteli kubwa za kitalii pamoja na makampuni mbalimbali ya utalii hapa nchini na wengine kujiendeleza zaidi katika makampuni ya nje ya Tanzania katika soko la dunia kutokana Lugha zaidi ya saba zinazo fundishwa chuoni hapo.
Comments
Post a Comment