WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA ARUSHA, WAOMBEWA KUSHINDA GOLI 10 KWENYE KILA MCHEZO WAO.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Timu ya Al Barakah FC ni timu ya Mpira wa miguu yenye maskani yake ukanda wa Magharibi mwa Tanzania, Ni timu inayo waunganisha wafanyakazi wa Benki ya CRDB katika ukanda huo wa Magharibi unaojumuisha mikoa 4 ya ukanda huo ambayo ni Shinyanga, Tabora, Geita na Kigoma.
Timu ya Al Barakah FC imeundwa mahususi kupitia kitengo cha Islamic Baking kutoka CRDB BANK, ikumbukwe CRDB ni Benki inayomsikiliza Mteja yenye kaulimbiu ya "ULIPO TUPO", lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii kile kinachokuwa kinapatikana katika faida ya biashara yao katika sekta ya huduma za kifedha hapa Nchini na nje ya Nchi.
Wakiwa Jijini Arusha kujiandaa mechi zao mbalimbali wachezaji wa Timu ya Al Barakah FC waliona ni vyema kujumuika kwa pamoja na kuwapa faraja watoto yatima wa kike wanao lelewa katika kituo cha kiislamu cha Rahma Orphanage Arusha Tanzania, kilichopo Halmashauri ya Arusha Dc katika Mji mdogo wa Ngaramtoni.
Wakiongozwa na Meneja Rasilimali watu wa CRDB Kanda ya Magharibi Ndg, Benjamin Ngayiwa, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Kitengo cha Islamic Banking Ndg, Rashid Rashid, ambapo wamewaza kukabidhi msaada huo wa vitu mbambali kwa watoto hao yatima katika kituo cha Rahma Orphanage Arusha.
Akikabidhi msaada huo Ndg, Benjamin Ngayiwa, ameeleza kuwa Benki ya CRDB imekuwa na Desturi ya kuitazama jamii katika nyanja mbalimbali ili kuweza kuisaidia kutokana na faida wanayo ipata kama benki ambapo misingi hiyo imeasisiwa na viongozi wao wa juu wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg, Abdulmajid Nsekela.
"Msaada huu umetolewa na wachezaji wenyewe ambao pia ni watumishi wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi lakini pia tumeungwa mkondo na Mkuu wa Kitendengo cha Islamic Banking, Ndg, Rashid Rashid, ili kuendelea kusaidia watoto hawa yatima ambao wanamahitaji mengi ya msingi". Amesema Ngayiwa.
"Hadi kufika hapa tuliweza kuwasiliana na mashehe wa Msikiti wa Mtendeni Jijini Arusha na wao waliona ni vyema msaada huu tukiuleta hapa Rahma Orphanage ambapo nyie mnawalea watoto hawa yatima wakike, Niwaombe na wadau wengine kuendekea kuisaidia jamii pindi wanapo guswa maana sisi tunaojaliwa kupata tuwe faraja kwa wenye shida hasa yatima". Ameelza Ngayiwa.
Timu hiyo ya Al Barakah FC imetoa msaada wa vyakula pamoja na mahitaji mengine ya msingi, ambapo imekabidhi Mchele Kg 100, Sukari Kg 50, Mafuta ya kupikia Lita 20, Sabuni ya unga pamoja na mafuta ya kupakaa mwilini.
Akitoa neno la Shukrani Bi, Sauda Omary, ambaye ni matroni katika kituo hicho cha Rahma Orphange Arusha ameweza kuwashukuru wachezaji wa Al Barakah Fc pamoja na benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kuwa msaada huo ambapo amesema umekuja wakati muhafaka.
Pia Sauda ameeleza kuwa kituo hicho kina jumla ya watoto yatima wakike 27 na bado wanayo mapungufu mengi ambapo waendelea kuimba benki ya CRDB kurudi tena kuwatazama kwa mara nyingine pia ameomba na wadau wengime kuiga mfano huo wa timu ya Al Baraka FC kwa kutoa fedha zao wenyewee mfukoni na kusaidia watoto yatima katika jamii.
Aidha Watoto hao wameweza kushusha dua maalum ya kuiombea timu hiyo ya Al Baraka Fc kushinda mechi zake zote itakayo kuwa inashiriki kwa kufunga magoli 10 na kuendelea kufanya vizuri katika michezo yao popote nchini.
Comments
Post a Comment