JIJI LA ARUSHA LAPOKEA VITI VYA WALEMAVU KUTOKA CONSERVATION FOUNDATION TANZANIA.

 MKURUGENZI AAHIDI KUTENGA MILIONI 20 ILI KUWEZA KUPUNGUZA CHANGAMOTO HIYO, AWAOMBA WADAU MBALI MBALI IKIWEMO TATO KUCHANGIA.

Na Lucas Myovela - Arusha.


Halmashauri ya Jiji la Arusha leo Disemba 14, 2023 imepokea msaada wa viti maalumu kwa walemavu vipatavyo 10 ( Viti vya Mwendo kasi ) kutoka katika Taasisi ya Kijamii ya Conservation Foundation Tanzania ( CFT ) Vyenye thamani ya Shilingi milioni tano na nusu za kitanzania.


Akipokea Msaada huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Juma Hamsini amesema waliomba msaada huo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Jijini Arusha kutoka kwa mdau huyo kutokana na uhitaji uliyokuwepo wa viti vya mwendonkasi kwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo, kwenye Zahati na Hosptali za Jiji hilo pamoja na baadhi ya familia zinazo ficha watoto walemavu na kisha kuanza kuomba msaada.


Hamsini ameeleza kuwa mbali na maombi mengi ya watanzania wenye watoto walemavu pia kuna ulemavu wa ukubwani ambao unaweza kumpata mtu yeyote pia na wale wagonjwa wa kisukari ambao imefikia hatua ya kushindwa kutembea na mahitaji hayo yote yanakusanywa na maendeleo ya Jamii na wao kama halmashauri wanaangalia sehemu zenye umuhimu zaidi.

 

"Bado tuna uhitaji wa viti hivi maalumu ( viti vya mwendo kaso ) kwenye jamii hizi, niwaombe watu wenye uwezo na utayari wa kuisaidia jamii waisaidie, Hapa Arusha tuna mahiteli mbali mbali, Taasisi mbali mbali za utalii ikiwemo TATO pamoja na Taasisi nyingine wanayo nafasi ya kuisaidi Serikali kwa kuangali shida zilizopo kwenye jamii". Amesema Hamsini.


"Sisi kama Halmashauri nikweli tunakusanya fedha lakini pia tunabajetiwa katika maeneo mengi sasa haya yanayo jitokeza kwenye jamii hapa nchini niwaombe watanzania kwa pamoja tushikane kama taifa maana ubitaji bado ni mkubwa hasa huko katika hosptali zetu kuwapelekea wagojwa wodini n.k". Aliongeza Hamsini.


"Pia ikumbukwe Arusha tunao uwanja wa ndege na wenda kunawagonjwa wanao safiri kwa haraka wanahijai viti hivi, Niwaombe Conservation Foundation kutokuchoka kusaidia jamii hapa nchini na katika maeneo mengine". Alisisitiza Hamsini.


Aidha Mkurugenzi Hamsini aliweka bayana mikakati kabambe ya kuounguza changamoyo hiyo katika Jiji la Arusha kuwa wamelidhia kwa pamoja na baraza la Madiwani kuanzia mwaka wa fedha 2024 / 25 kutenga fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha Shilingi Milioni 20 kwa ajili yakusaidia watu wenye ulemavu.

Bi, Rose Bekker, ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Conservation Foundation Tanzania Mrs. Jan Ramoni, amesema taasisi yake imetoa jumla ya viti 10 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5 ambapo kwa kiti kimoja kina gharimu kiasi cha shilingi laki tano na nusu za kitanzani.


"Tulipata ombi la viti vya walemavu na leo hii tunakadhi viti 10 vya mwendo kasi kwaajili ya welemavu na sisi hatuta ishia hapa katika kutoa msaada huu tupo tayari kuendelea kuisapoti Serikali yetu kwa kadri tunavyo weza ili kusonga pamoja kama taifa". Alisema Bekker.


Aidha Bi Rose amesisitiza kuwa taasisi yake itaendelea kushirikiana na Serikali hususani katika kusaidia watu wenye uhitaji wa viti mwendo na kuomba mashirika mengine na Taasisi zingine kuisapoti serikali ili kuweza kutokomeza na kuondoa changamoto mbalimbali katika jamii.


Picha: (Kulia) ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini, Akipokea msaada viti 10 kutoka kwa Mwakilishiwa wa Taasisi Conservation Foundation Tanzania Bi, Rose Bekker ( Kushoto).

Comments