MAHAKAMA YAAMURU KESI HIYO IANZE UPYA KUSIKILIZWA 2024.
Na Lucas Myovela _ Moshi_ Kilimanjaro.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi,Lilian Mongella amesema Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi la Mji wa Moshi lilikosea kisheria wakati walipotembea eneo la tukio la mgogoro wa Ardhi wa familia maarufu katika Mji wa Moshi ya Mereale na kusema maamuzi hayo ni batili hivyo aliagiza Baraza hilo kusikiliza upya kesi hiyo.
Akisoma hukumu hiyo leo katika kesi namba 51/2023 ya mlalamikaji wanandugu Frank Mareale dhidi ya Ackley Mareale Jaji Mongella alisema baada ya kupitia ushahidi na maamuzi ya Baraza la Nyumba na Makazi la Mji wa Moshi chini ya Uenyekiti wa Reginal Mtei yaliyotolewa mei 5 mwaka huu na kusema kuwa maamuzi hayo yalikuwa na kasoro za kisheria.
Jaji Mongella alisema kuwa moja ya mapungufu katika maamuzi ya Baraza ni pamoja na kushindwa kuonyesha au kurekodi mipaka ya ardhi ya ekari mbili inayogombaniwa na wanafamilia hao hivyo ametengua maamuzi hayo na kuamuri kesi hiyo isikilizwe upya chini ya Mwenyekiti Mwingine.
Alisema katika mapitio ya maelezo ya mashahidi wa kesi hiyo katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi hakuona kama Baraza hilo limeonyesha mipaka ya eneo la mgogoro na kusema kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
"Nimeamua kesi hii ya wanafamilia wa Mareale isikilizwe upya kwa sababu Baraza la Ardhi lilikosea kisheria kwa kushindwa kuonyesha mipaka ya ekari mbili inayogombaniwa". alisema Jaji Mongella.
Katika kesi iliyofunguliwa na Frank Mareale katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi katika Mji wa Moshi, alikuwa na madai matatu moja wapo ni ombi la kwanza Baraza hilo litamke kuwa eneo la ekari mbili yeye ni mmiliki halali, Pili Baraza litoe amri ya kufukuliwa mwili wa marehemu mama yake mdogo Verenica Mareale na pia alipwe gharama za kesi.
Mei 5 mwaka huu chini ya Uenyekiyi wa Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi ,Reginald Mtei lilitupilia mbali madai ya Frank Mareale na kusema kuwa Ackley Mareale ni mmiliki halali wa eneo hilo na sio vinginevyo.
Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa Ackley Mareale,Julius Semali alisema kuwa hana pingamizi na uamuzi wa Mahakama kwani ana uhakika kuwa mteja wake ni mmiliki eneo hilo kwa kuwa mama yake alipata kihalali na alizikwa ene hilo na kurudishwa tena katika Baraza hana shaka na uamuzi wa awali na kusema kuwa usikilizwaji mwingine utathibitisha kuwa haki ya mtu huwa haipotea ila inacheleweshwa.
Naye Wakili wa frank Mareale,Modest Njau aliishukuru Mahakama Kuu kwa uamuzi wake wa kuiagiza Baraza la Ardhi Nyumba na MakaziMoshi kusikiliza upya kesi hiyo na aliamuru Mwenyekiti wa Baraza na wajumbe wake wabadilishwe.
Njau alidai Mahakama Kuu iliona jinsi haki ilivyokuwa ikitaka kuchezewa katika usikilizwaji wa awali nay eye na mteja wake wameridhika na maamuzi hayo.
Comments
Post a Comment