AMTAKA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHWA KUTOYUMBISHWA NA WANASIASA ASIMAMIE MSIMAMO WA MIKATABA INAVYO TAKA.
"JENGENI MAJENGO YA KISASA KILA KITU MNACHO ACHENI KUYUMBISHWA NA WANASIASA WASIYO JITOSHELEZA".
Na Lucas Myovela - Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe, John Mongella amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini kutoyumbishwa na mikataba mibovu iliyo ingiwa na wajenzi ambayo inaigharimu serikali kwa kuchochewa na wanasiasa ambao waapotosha ukweli.
Mongella ameyasema hayo Jijini Arusha wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa stendi mpya eneo la Themi iliyopo kata ya Themi ziara hiyo aliyo ifanya Disemba 22, 2023 na kujionea hali halisi ya uwazwaji wa ujenzi huo wa stendi mpya na yakisasa.
Akikagua eneo hilo la ujenzi wa Stendi Mpya Rc Mongela ameagiza mchoro wa stendi hiyo uboreshwe upya ikiwemo msingi wa vibanda vitakavyojengwa hapo uwe wa ghorofa ili iwe ya kisasa zaidi na kuwa ya mfano hapa nchini ikiwemo kutengwa eneo maalumu la kupandwa miti kwaajili ya uboreshaji wa mazingira na kupata mahali pa kupumzikia wa safiri pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha pia Rc Mongela amemueleza Mkugenzi wa Jiji hilo Juma Hamsini kuwa aache kusikiliza mtu yeyote kuwasikiliza hasa ambao hawajui mipango ya serikali ya kuboresha maisha ya watanzania na badala yake asimamie msimamo wa serikali hasa mikataba inayoingiwa na watu mbalimbali pale inapo keukwa.
“Mkurugenzi unayumba kwanini, mnaweweseka tu kila kitu mnacho hamtaki kumaliza mgogoro ule wa stendi ndogo, Sisi viongozi tumewekwa hapa Kwa maslahi mapana ya wana Arusha na siyo maslahi ya wanasiasa". Amesema Mongela.
"Hatujengi nchi hii na Taifa hili kwa kumwangalia mtu, Tusijizimishe data au kujitoa ufahamu sisi wengine hatupo kwenye mihemko hiyo ya kutafuta kiki ambazo hazina maana yeyote wala maslahi ya taifa letu, Mhe, Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anaangaika kulijenga taifa letu na sisi aliyetupa dhamana ya kumsaidia lazima tusimame nae muda wote”. aliongeza Mongela.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji Arusha Juma Hamsini ameema Halmashauri hiyo inajenga stendi hiyo mpya ili kupunguza msongamano wa daladala uliyopo hivi sasa na zile zinazopaki kando kando ya barabara kuu eneo la Kilombero na stendi ndogo.
"Nimepokea maelekezo ya Mkuu wangu wa Mkoa niwaombe sana wafanyabiashara wa Jiji la Arusha kujisajili katika mfmo huu mpya wa TAUSI ndiyo utawasaidia wote kuondokana na changamoto ya mgogoro wa stendi ndogo ambao unaofukuta hivi sasa na Mimi siko tayari kusikiliza maneno ya kisiasa kwa maslahi ya mtu fulani tutachukua hatua zaidi katika jambo hilo la mgogoro wa stendi ndogo na kulimaza kabisa". Alisema Juma Hamsini.
Comments
Post a Comment