SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA FEDHA TAWIRI ILI KUTOA MAFUNZO ZAIDI KWA WATAIFITI.

KUCHIMBA MABWAWA YA MAJI HIFADHINI ILI KUPUNGUZA MUINGILIANO WA WANYAMA KWENUE MAKAZI YA BINADAMU WAKATI WA KIANGAZI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Akifungua kongamano la 14 la Kimataifa la Kisayansi linalofanyika kwa siku tatu Jijini Arusha na kukutanisha watafiti kutoka nchi 22 za ndani na nje ya nchi, Waziri wa Maliasili,Angellah Kairuki kwaniaba ya Makamu wa Rais,Dk, Philip Mpango alisisitiza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kudhibiti muingiliano wa wanyama na binadamu.


Waziri Kairuki ameelez kwamba Serikali itaendelea kuweka fedha za kutosha kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watafiti wa kizazi kijacho cha watanzania wenye uwezo na ujuzi maalumu katika fani za upelelezi sanjari na teknolojia zinazoibukia za uhifadhi kusaidia ufuatiliaji na udhibiti wa spishi ngeni vamizi (AIS).

Pia Kairuki ameongeza kuwa Wakati huo huo ,serikali imeridhia mikataba kadhaa ya kimataifa ikiwa mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama na Wanyama walio Hatarini Kutoweka (CITES), Mkataba wa Bioanuwai (CBD), Urithi wa DuniaMkataba, na Mkataba wa Ramsar pamoja na mikataba ya kikanda/mikataba ikijumuisha Mkataba wa Afrika Mashariki (Kifungu cha 114 cha Utalii na Kifungu cha 115 kuhusu usimamizi wa wanyamapori).


"Mwingiliano wa binadamu na wanyamapori umeongezeka kutokana na shughuli za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na makazi, kilimo na malisho ya mifugo ambapo kutokana na mipango duni ya matumizi ya ardhi karibu na maeneo ya hifadhi, kuziba kwa shoroba za wanyamapori,uvamizi wa viumbe ngeni, mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia za wanyamapori". Amesema Kairuki.


"Teknolojia na uvumbuzi vina jukumu katika harakati za kudhibiti matukio ya uvamizi wa wanyama na binadamu na kusisitiza kuwa TAWIRI imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha migogoro inapunguzwa kote nchini kupitia mafunzo ya tovuti kwa jamii zinazopakana na maeneo ya hifadhi , ufuatiliaji wa mienendo ya wanyamapori na katika baadhi ya matukio kuwarudisha wanyamapori kwenye maeneo yanayolindwa kutoka kwa jamii". Ameongeza Kairuki.


" Serikali itatenga fedha maalum kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi kuu ya mamalaka hiyo , ukarabati wa majengo katika vituo vya utafiti pamoja na ununuzi wa vifaa vya utafiti,lakini pia kutoa elimu kwa vijiji vinavyozunguuka hifadhi ikiwemo kuchimba mabwawa ya maji ndani ya hifadhi ili kudhiti wanyamapori wasitoke hifadhini kwenda kutafuta maji nyakati za kiangazi". Amesisitiza Kairuki.

Waziri Kairuki ameeleza kuwa kuongezeka kwa migogoro ya binadamu na wanyamapori katika miaka ya hivi karibuni ambayo baadhi yake inahusishwa na uharibifu wa mazao, majeraha au vifo vya binadamu, uharibifu wa mali, uharibifu wa mifugo, na mauaji ya kulipiza kisasi ya viumbe muhimu kama vile tembo na simba. 



"Serikali imedhamiria kuimarisha maisha ya pamoja ya wanyamapori na binadamu, ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii kuaandaa mkakati wa Dharura na wa kati wa kupunguza Migogoro ya Binadamu na Wanyamapori katika Taifa na thmini ya korido za wanyamapori". Ameeleza Kairuki

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri Dkt,Eblate Mjingo alisema kongamano hilo ni muhimu kwaaajili ya kutoa na kujadili na kisambaza matokeo ya kitafti yaliyofanyika miaka miwili iliyopita ili kusaidia uhifadhi na kuendeleza utalii ili kuhakikikisha changamoto ya binadamu na wanyamapori haswa tembo zinadhibitiwa.


Kupitia filamu ya Royal Tour serikali imeongeza idadi ya watalii kutoka 1,711,625 (watalii wa ndani- 788,933 na watalii wa kimataifa- 922,692) mwaka 2021 hadi 3,818,180 (watalii wa ndani-2,363,260 na watalii wa Kimataifa - 2020,2024) ambapo hadi k kufikia 2025 idadi ya watalii itaongezeka na kufikika milioni 5 .


Takwimu za utafiti kutoka TAWIRI zimeonyesha kuwa jumla ya wilaya 44 kati ya 81 za Tanzania Bara zinaongoza kwa migogoro ya binadamu na wanyamapori.






Comments