WAFANYABIASHARA ARUSHA WAZIDI KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAUSI KUEPUKA MADUKA YAO KUPIGWA MNANDA.

ATOA UFAFANUZI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO PAMOJA NA SHUGHULI ZA SERIKALI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini ameeleza kwamba katika zoezi la kuwasajili wafanya biashara wote wa Jiji la Arusha ambao ni wapangaji kwenye maduka ya Halmashauri hiyo wamejitokeza kwa wingi kujisajili katika mfumo mpya wa TAUSI ambao unamuweza mfanyabiashara kutambulika kitaifa endapo atajisajili.

Hamsini ameeleza kuwa katika zoezi hilo wafanyabiashara wamejitokeza kwa wingi baada ya halmashauri hiyo kutoa elimu na kutuma wataalamu kuwafata wafanyabiashara na kuwasajili katika maeneo yao ya kibiashara lengo likiwa ni kufikisha huduma karibu kwa wananchi ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo zoezi hilo litakapo kwisha muda wake.


"Lengo la Serikali ni kila mfanya biashara ajisajili katika mfumo huu wa TAUSI na kulipa kodi iliyo wekwa na serikali na mfumo huu unamuweza mfanyabiashara popote alipo nchini kutambulika na niwatoe hofu wafanyabiashara huu usajili huu siyo wa halmashauri ya Jiji la Arusha ni mfumo uliyo wekwa na Serikali na sisi kama wasimamizi lazima tuhakikishe serikali inapata kodi kwa wakati ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi". Amesema Hamsini.


"Pia niwapongeze wafanyabiashara ambao wameweza kujisajili kwakweli ni wengi sana ingawa kulikuwa na baadhi ya viongozi wachache walitaka kupotosha ukweli lakini nimeona wafanya biashara wengi wameelewa serikali inahitaji nini kwao hasa katika kipindi hiki ambapo wanatakiwa kulipa kodi mpya serikali". Aliongeza Hamsini.

Akitoa ufafanuzi huo wa zoezi hilo la kujisajili kwa mfumo wa TAUSI Mkurugenzi Hamsini ameeleza licha ya wafanya biashara hao kujisajili pia kumekuwa na changamoto ya wafanyabiashara hao kutokuwa na mikataba ya vibanda vyao pamoja na leseni za biashara wanazo zifanya ambapo hivi sasa ameamua kulifatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha kila mfanya biashara analeseni husika ya biashara yake.


Pia Hamsini ameeleza kwamba endapo muda wa kujisajili utakapo kwisha maduka yote yanayo milikiwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha yatapigwa mnada kwa kupitia mfumo huo huo wa TAUSI na mtu yeyote anaruhusiwa kuomba duka hilo kwa ajili ya kufanya biashara ambapo pia akipata atajaza mkataba uliyopo sasa na kulipa kodi mpya iliyopangwa.

"Siku zikiisha za kujisajili katika mfumo huu wa TAUSI tutayapiga mnada maduka yote ambayo hayana mkataba huu mpya na mfanyabiashara ukikuta rangi nyekundu kwenye namba ya duka lako tambua tayari umejisajili ila ukikuta namba ya duka lako lina rangi nyeupe jua linapigwa mnada mtu yeyote anaruhusiwa kuomba duka hilo na kupata". Amesema Hamsini.


Maduka yanayotakiwa ya Halmashauri ya Jiji la Arusha yanayo takiwa kufanyiwa usajili wa mikataba mipya kwa njia ya TAUSI na kuwa na lesini ya biashara husika ni maduka ya Stendi ndogo, Morombo, Kijenge Krokoni, Rangers Safari ya Zamani na Mpya, Stendi Kuu, Soko Kuu, Olmoti, Kirombero, Mbauda Sanawari, Mnara wa Mwenge, Olmetejo, pamoja na Suye.


Awali akitoa ufafanuzi wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli za Serikali kipindi cha Julai hadi Disemba 2023, Mkurugenzi Hamsini ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023 - 2024 Halmashauri imeendelea kusimamia na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kupitia mapato ya ndani na ruzuku ya Serikali kwa fedha zilizo tolewa katika kipindi chwa mwaka wa fedha 2022 - 2023 na fedha za mapato ya ndani zilizo tolewa mwaka 2023 - 2024.


Pia maeeleza Shughuli mbali mbali na majukumu yanasimamiwa ipasavyo na kutekelezwa katika sekta zote ikiwa ni Sekta ya utawala, Sekta ya viwanda na biashara, Sekta ya Mipango Miji, Sekta Elimu ya Msingi, Sekta Elimu Sekondari, Sekta ya Afya, Sekta ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Sekta ya Ujenzi.

Comments