WAZIRI UMMY AZITAKA HOSPTALI ZA MIKOA NA RUFAA KUTOA TIBA KEMIA KWA WANANCHI.

 AIPOGEZA HOSPTALI YA MOUNT MERU ARUSHA KWA KUTOA HUDUMA BORA KUSHINDA HOSPALI ZA BINAFSI.

Na Lucas Myovela- Arusha.


Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu ameagiza Hospitali zote za Mikoa za Rufaa nchini kuhakikisha zinatoa Tiba Kemia kwa lengo la kumpunguzia mgonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo Jijini Dar es Salam.

Mwalimu alisema hayo Leo Disemba 30, 2023  Jijini Arusha mara baada ya kutembelea Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kuzindua maabara ya kisasa ya hospital hiyo.


Alisema Tiba Kemia hutolewa katika Hospital ya Rufaa ya Muhimbili na Ocean Road tu na wagonjwa wamekuwa wengi kote nchini hivyo ni wakati wa Hospital za Rufaa za Mikoa kutoa huduma hiyo ili kuwapunguzia wagonjwa umbali mrefui kufuata tiba hiyo Jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo alisema hatua iliyofanywa na Hospital ya Rufaa ya Mount Meru Mkoani Arusha ya kutaka kuanzisha huduma ya Tiba Kemia ameiunga mkono na kuzitaka hospital nyingine za Rufaa za Mikoa kuiga mfano wa hospital hiyo.


Alisema Hospital za Rufaa ambazo Madaktari Bingwa hawapo wanapaswa kuongezwa ili hospital hizo ziweze kutoa huduma tiba kibingwa ili wananchi waweze kufurahia huduma katika hospital za serikali.

Waziri aliusifu uongozi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru chini ya Mganga Mfawidhi Dkt Alex Ernest kwa usafi,utoaji wa huduma safi na uwepo wa dawa na vifaa tiba na na Utendaji kazi na usimamizi wa dhati kwa watumishi na kutoa huduma kwa wananchi na kusema kuwa hospital nyingine zinapaswa kuiga mfano huo.


Alisema Dkt Alex ni mfano wa madaktari Bingwa kote nchini kwani yuko karibu na watumishi wote wa hospital hiyo na anatatua changamotozao zote hivyo Madaktari wengine wa Hospital za rufaa wanapaswa kuiga mfano.

"Nimeridhishwa na usafi na utoaji huduma katika Hospital hii ya Mount Meru kwani nimejionea mwenyewe na mnastahili pongezi na msibweteke hakikisheni mnaongeza kasi kwa maslahi ya wananchi’". alisema Mwalimu.


''Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan hatudai kwani emashafanya kazi yake ya kutoa fedha katika huduma ya Afya mamilioni ya fedha kote nchini hivyo ni wajibu wetu kutoa huduma safi kwa wananchi''alisema 

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt, Charles Mkombachepa alimweleza Waziri kuwa Mkoa wa Arusha kwa sasa una vituo vya afya 431 hadi disemba mwaka huu na serikali inamiliki vituo 259 sawa na asilimia 60 ukilinganisha na mwaka 2021/22 ambapo kulikuwa na vituo 241 sawa na asilimia 57 na taasisi za dini na binafsi zinamiliki vituo vya afya 172 sawa na asilimia 39.


Dkt, Mkombachepa alisema kuwa kuna hatua kubwa sana imepigwa katika kujenga na kuimarisha miundambinu ya kutolea huduma ya afya kwani katika 2021/22 kulikuwa na hospital 6 za Halmashauri na kufikia Disemba mwaka huu Halmashauri zote saba Mkoani Arusha zina Hospital na zote zimeanza kutoa huduma.

Alisema mwaka 2021/22 kulikuwa na vituo vya afya 37 na mwaka 2023/24 jumla ya vituo afya 3 vimeongezwa na kufikia 40,mwaka 2021/22 kulikuwa na zahanati 194 na mwaka 2023/24 zimeongezeka na kufikia zahanati 211,mwaka 2021/22 kulikuwa na vyumba vya upasuaji 17 ukilinganisha na mwaka 2023/24 kuna vyumba vya upasuaji 21 kwa vituo vya serikali.   

Naye Mganga Mfawidhi wa Hisptal ya Mount Meru Dkt, Alex Ernest alimweleza Waziri Mwalimu kuwa Hospital ya Rufaa ya Mount Meru inanunuwa dawa MSD kwa fedha taslimu,wazabuni na wafanyakazi wa Hospital hiyo hawana deni nao kwa kuwa kila kitu wanachostahili kulipwa wameshalipwa au wanalipwa kwa wakati.


Dkt Ernest alisema malewngo ya mkusanyo ya mwaka 2021/22 yalikuwa shilingi bilioni 5 lakini hospital hiyo ilivuka malengo na kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 6.


Alisema katika malengo ya makusanyo ya fedha katika kipindi cha julay mwaka 2023/24 HGospital hiyo imepanga malengo ya kukusanya shilingi bilioni 7 lakini kwa kipindi cha miezi cha miezi sita hospital hiyo imeshakusanya zaidi ya shilingi bilioni 4 na huenda malengo waliyokusudia watatimia na ikibidi kuyavuka bila ya kikwazo.













Comments