DIWANI ALIA KUKWAMISHWA, ADAI HALMASHAURI VIKAO HAVIFANYIKI KWA WAKATI VINAFANYIKIA HOTELINI.

RC SENDIGA ATOA SIKU 5 KWA DC KUMPELEKEA MEZANI KWAKE MAJIBU.

ATAKA WANANCHI KUPEWA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI MAANA RAIS SAMIA ANATOA FEDHA ZA MAENDELEO.

ATUMA SALAMU KWA AFISA ELIMU KUKAA KWENYE KITI CHAKE NA AENEE ASIPWAYE. 


Na Lucas Myovela - Mirerani.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Queen Sendiga amempa siku tano Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro,Suleman Serera kuhakikisha shule ya sekondari ya kata ya Endiamtu inaanza kujengwa ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mtendaji wa Kata Mirerani,ujenzi wa Maabara na ukarabati wa majengo shule za msingi Mji wa Mirerani unafanyika haraka iwezekanavyo na sio vinginevyo.


Sendiga alisema hayo katika Mji wa Mirerani wakati akizindua kampeni ya kukabiliana na upungufu wa madawati Mkoa wa Manyara na kusema kuwa suala la baadhi ya watu kukwamishana na kuingiza siasa katika mambo ya maendeleo hataki kujua wala kusikia katika Mkoa wa Manyara.


Alisema inasikitisha kusikia kuwa maabara ya shule ilizinduliwa kipindi cha awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na bajeti yake ilipitishwa lakini hadi leo hakuna ujenzi na pia ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika hilo uko kimya,Ofisi ya kata hakuna Mirerani na ukarabati wa shule unashindwa kufanyika kisa watu wanakwamisha jitihada za serikali katika maendeleo kisa siasa kitu ambacho amekikemea vikali na kusema  haliwezekani kuendelea chini ya uongozi wake kama Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Sendiga  alisema hayo baada ya Diwani wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} Lucas Chimba kutoa malalamiko hayo baada ya kupewa nafasi ya kusalimia katika uzinduzi huo wa kampeni ya "Mpe Maua Atabasamu Asome Kifalme" na kusema kuwa inasikitisha baadhi ya watu wanamkwamisha katika kuunga mkono jitihada za Rais DKt Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo katika kata ya Mirerani na Endiamutu.


 "Nimesikia kilio cha Diwani wa kata hii ndugu yangu Chimba, Mkuu wa wilaya ninakupa siku tano kuhakikisha vitu vyote vilivyozungumzwa vinapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuanza mara moja ujenzi wa shule mpya ya sekondari na kuhakikisha majengo haya ya madarasa yanafaniwa ukarabati haraa". Alisema Sendiga.


"Mkurugenzi ninakuagiza kwa Afisa elimu wako umwambie akae kwenye kiti atoshee aache kupwaya maana serikali hii ya awamu ya sita inatoa fedha za elimu bure ninatakankujua changamoto ya shule zote zenye uchakavu na zifanyiwe ukarabati l, Wazazi hawa wamesimamia maandiko ya kuijaza dunia na sisi kama viongozi lazima tuwawekee miundo mbinu sahihi ya watoto kupata elimu bora". Aliongeza Sendiga.


Mkuu wa Mkoa alisema inasikitishakuona maabara toka enzi za Rais Mstaafu Kikwete bado inasuasua,ujenzi wa shule ya sekondari hakuna,Mirerani hakuna ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo ni aibu na suala hilo linapaswa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo.


Alisema katika kuhakikisha hilo amelivalia njuga alitoa mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata na kumwambia Diwani Chimba ahakikishe anatafuta kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa shule na ofisi ya kata kwani vyote ni muhimu katika Mji wa Mirerani.


Sendiga alilitaka Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Simanjiro kujitathimni haiwezekani bajeti inapitishwa lakini utekelezaji hakuna hilo halikubaliki na kama ni hivyo basi Baraza hilo halipaswi kuwepo kwani linapaswa kuvunjwa.


Alisema kila Diwani anapaswa kuwajibika katika kata yake ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya CCM na kama hilo halifanyiki basi madiwani wote wanapaswa kuwajibika kwa wananchi waliowachagua kwa kuwa hawatoshi.


"Nataka kila Diwani awajibike katika kata yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anatekeleza ilani ya CCM na kama hilo huwezi hutoshi na unapaswa kuwajibishwa". Amesema Sendiga.

Awali Diwani kata hiyo Mhe, Luca Chimba alisema kuwa kata yake na kata ya jirani ya Mirerani inakwamishwa katika maendeleo na wanasiasa kwa malengo yao binafsi na inasikitisha kuona bajeti inatengwa lakini haitekelezeki kwenye kata yake ili kuwasaidia wananchi.


Chimba alimwomba Mkuu wa Mkoa kumsaidia kwa hilo maana maabara toka enzi ya serikali ya awamu ya nne haijajengwa wakati bajeti ilipitishwa ikiwemona shule na kibaya zaidi hata ofisi ya kata Mirerani hakuna.


"Tuna muda mrefu hatujafanya vikao vya mji mdogo mirerani kwasasa vikao hivi vimekuwa vikifanyika hotelini kitu ambacho akileti mafaniko katika maendeleo na sisi kama madiwani hatupati faida yeyote ya kuwasilisha koro za wananchi wetu". Amesema Chima.


"Kata yangu haipewi fedha za maendeleo na sijui nikwanini ila kata zingine zinapewa fedha za kutosha ila kata hii sishirikishwi kupewa fedha za maendeleo, tumekuwa tukishirikiana na kata za jirani kuona namna bora ya kuwasaidia wananchi wetu maana mwenyekiti wetu wa baraza la madiwani haiti vikao kwa kigezo kwamba halmashauri haina fedha". Aliongeza Diwani Chimba.


Aidha pia Mhe, Chimba alisema kwa uchungu mkubwa sana  kuwa yupo tayari kujivua udiwani endapo kama anayosema hayana ukweli na hayata fanyiwa kazi maana wananhi wake wanateseka sana hasa katika swala zima la elimu kutokana na majengo hayo ya madarasi niya zamani tika enzi za uhuu wa nchi hii kitu ambacho siyo sahihi.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Simanjiro, Gracian Makota akijibu tuhuma hizo alisema halmashauri yake haina upendeleo na inatekeleza kwa mujibu wa bajeti iliyopo na kuhaidi kutia ushirikiano kwa diwani Chimba kuanzia sasa.


Makota alimwomba Diwani Chimba kushirikiana na ofisi yake katika kuhakikisha maabara inaanza ujenzi na shule ya sekondari kata ya Endamtu nayo inajengwa.


Comments