WATOTO WENYE UHITAJI 150 WATAPATA MSAADA HUO ILI KUEDELEA NA MASOMO YAO.
Na Lucas Myovela -Arusha.
Wanafunzi 75 kati ya 150 wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji wa shule tatu za Msingi Kata ya Moshono Jijini Arusha wamefanikiwa kupata msaada wa vifaa vya shule kutoka kwa Diwani wa kata hiyo Miryam Kissawike.
Diwani Kissawike baada ya kugawa vifaa hivyo vya shule kwa Watoto hao vikiwemo madaftari,kalamu,begi na vitu vingine muhimu alisema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwavutiawatoto wengine waliokuwa katika hali hiyo waweze kwenda shule bila ya kuwa na visingizio.
Alisema wakati serikali imeondoa ada katika shule yeye kama Diwani ameamua kuwanunulia vifaa vya shule Watoto wa shule za msingi wa darasa la kwanza na baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuingia kidatu cha kwanza.
Diwani alisema Rais Dkt, Samiaa Suluhu Hassan ameshafanya kwa sehemu yake juu ya kuboresha elimu kwa shule za msingi katika kata yake nay eye kama kiongozi wa jamii ameamua kutekeleza kwa vitendo kuwanunulia wanafunzi vifaa vya shule ili waweze kupata elimu ya kuweza kujikomboa kimaisha.
Alisema wanafunzi wa shule tatu za msingi katika kata yake ikiwemo shule ya msingi Moshono,Wema na Olkerien wamenufaika na msaada huo wenye gharama ya zaidi ya shilingi 375,000 na lengo ni kuwafikia wanafunzi zaidi ya 150 katika kata hiyo wale wenye uhitaji maalumu.
‘’Nimeamua kuanza kutoa msaada kwa wanafunzi 150 na leo nimetoa kwa wanafunzi 75 na zoezi hili bado linaendelea na lengo nikuwafikia wanafunzi wote wenye uhitaji bila kujali idadi yao’’
‘’Nawaomba wadau wa elimu katika kata ya Moshono kujitoa na kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji kwani wanafunzi hao nao wanahitaji elimu lakini wanashindwa kwa kuwa wazazi wao hawana uwezo’’alisema Diwani Kiwassawike
Naye mzazi wa mmoja wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mery Mollel alimshukuru Diwani huyo kwa msaada huo na kusema kuwa kwa kiasi kikubwa umewasaidia wao kuwapa moyo wa Watoto wao kwenda shule.
Mollel alisema kiukweli hakuwa na namna ya kufanya baada ya mtoto wake kujiandikisha kwenda shule kwani aliweza kupata msaada wa unifomu ya shule tu na vifaa alishindwa kununuwa na msaada huo ulipokuja amefarijika sana.
Alisema na kuwataka watu wenye uwezo kuiga mfano wa Diwani katika kutoa msaada kwa wanafunzi wenye uhitaji kwani wako wengi lakini hawana uwezo hivyo wanahitaji msaada sana ili waweze kupata elimu.
Comments
Post a Comment