FRANONE MINING YATOA MADAWATI 100 KWA WANAFUNZI WASOME KIFALME.

RC SENDIGA AFUNGUKA MAZITO ATAKA WADAU KUIGA MFANO WA FRANONE MINING KUTOA KWA JAMII.

Na Lucas Myovela - Mirerani.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Queen Sendiga amezindua kampeni maalumu ya kukabiliana na upungufu wa meza na viti 4,664 kwa wqnafunzi wa Sekondari na Madawati 28,336 kwa wanafunzi wa shuke za msingi katika Mkoa wa Manyara ambapo kampeni hiyo maalumu ijulikanayo kwa jina la ‘’Mpe Maua Atabasamu Asome Kifalme ‘’ ambapo pia amewataka wadau wa mendeleo Mkoani hapo kumuunga mkono.

 Akizindua kampeni hiyo Leo Januari 26,2024 Kimkoa katika Mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro katika shule ya Msingi Mirerani na kuwataka wawekezaji wa sekta zote Mkoani Manyara,Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa sekta ya madini ya Tanzanite na taasisi za dini,umma na binafsi na wafanyabiashara wa mbalimbali kumuunga mkono katika jitihada za kumtaka mwanafunzi kusoma akiwa amekaa kwenye kiti.


Katika kampeni hiyo imeanza kwa utatuzi wa changamoto ya madawati katika shule ya msingi Mererani ambapo kampuni ya Franone Mining & Gems Co. Ltd imechangia madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni nane ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma wamekaa kwenye madawati kama wanafunzi wengine wanavyo soma lengo likiwa ni kuchangia katika sekta ya el8mu na kuunga juhudi za serikali ya awqmu ya sita katika kuikuza sekta ya elimu.


Rc Sendiga ameeleza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha katika Mkoa wa Manyara shilingi Bilioni 94 katika sekta ya elimu hivyo basi wadau wa elimu wanapaswa kumuunga mkono Rais katika jitihada zake za kuboresha elimu Mkoani Manyara kwa kuchangia madawati,viti na meza kwa wanafunzi.

"Leo hii nunekabidhi madawati haya 142 hapa shule ya msingi mirerani ambayo jumla yake ni milioni 11, Kipekee niwashukuru kampuni ya Franone kwa mchango wao mkubwa kwa jamii hii ya hapa mirerani ambapo wao pekee wamechangia madawati 100 na hayo mengingie 42 ni kutoka kwa wadau wengine niwaombe wasiishie hapa waendelee kujitoa kusaidia jamii na sisi kama serikali tunawategemea sana wawekezaji hawa maana wapo mstari wa mbele kujitoa katika jamii". Alisema Sendiga.


Aidha Rc Sendiga ameeleza kuwa Mkoa wa Manyara unakila sifa kutokana na upekee wake wa madini ya Tanzanite pamoja na kuongoza katika Michezo hivyo ni wajibu wadau popote walipo wahakikishe wanashirikiana vyema na serikali yao na kuiga mfano kutoka katika kampuni ya Franone ili kufanikisha maendeleo ya watu wa Mkoa wa Manyara na sio vinginevyo.

"Kwa namna yoyote ile huwezi kuacha kuwashukuru kampuni ya madini ya Franone chini ya wakurugenzi pacha hao Ndg, Onesmo Mbise na Francis Matunda kwa kuonyesha njia na nia njema katika kampeni hii pamoja na wadau wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} Wilaya ya Simanjiro Ndg, Kiria Laizer kutafuta wandau na kuanza mchakato wa kuchangia madawati haya ambayo leo hii yaenda kuondoa changamoto kwa watoto wetu". Amesema Sendiga


"Kampeni hii nimeizindua kwa mkoa mzima wa Manyara hapa Wilayani Simanjiro Mirerani ili kuhakikisha kila mwanafunzi wanakaa katika viti kupata elimu na ni kampeni ya wilaya zote saba za Mkoa wa manyara niwaombe wawekezani wengine katika maeneo mengine ya Mkoa wetu wa Manyara tuungane kwa pamoja kufanikisha hili’’. Ameongeza Rc Sendiga.

Picha: Kushoto ni Meneja wa Migodi ya Franone Mining ndg, Vitus Ndakize wakiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe, Queen Sendiga na Kulia ni Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Franone Mining Bw, Francis Matuda.

Kwa upande wake Meneja wa Franone Mining & Gems Co. Ltd Ndg, Vitus Ndaikize amesema kuwa kampuni ilifikia hatua hiyo ya kutoa msaada huo baada ya kusikia kuwa shule Kongwe ya Msingi Mirerani yenye wanafunzi 1,276 ikiwa na upungufu wa madawati ndipo wakurugenzi wa Franone walipoamua kutoa msaada huo wa madawati 100 maana wao kama wawekezaji wanaunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta elimu, Afya, Maji na barabara kwani ni wajibu wao kurudisha faida kwa jamii.


"Kwa kampuni yetu sio mara ya kwanza kutoa msaada kwa jamii inayo tuzunguka katika kuunga Mkono jitihada za serikali maana tunafanya hivyo mara kwa mara kutokana na mipango yetu ya kampuni tuliyo jiwekea na hata pindi tunapohitajika kufanya hivyo tunafanya bila kuwa na wasiwasi maana sote tunajenga nyumba moja ambalo ni taifa letu la Tanzania". Alisema Ndakize.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Suleman Serera alisema kuwa katika Wilaya hiyo shilingi bilioni 21 zimeletwa kwa ajili ya elimu hivyo basi wadau wa Maendeleo wanapaswa kumuunga mkono Rais kwa kutatua upungufu wa madawati katika wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.


Alisema kwasasa wadau wa elimu katika maendeleo kupiga marufuku siasa uchwara zinazo emezwa na baadi ya wanasiasa ambao wanataka kuchanganya siasa na maendeleo hawapaswi kupewa nafasi hivyo kinachongaliwa kwa sasa ni kukabiliana na upungufu wa madawati kuoitia kampeni hiyo maalum na kuhusu swala zimq la siasa zifanywe wakati ukifika.

"Mambo ya siasa katika maendeleo ya Wilaya yetu ya Simanjiro hayana nafasi na nawaomba wadau tumuunge mkono Mkuu wetu wa Mkoa katika kampeni yake hii ya kukabiliana na upungufu wa madawati Mkoani Manyara na mimi sitamfumbia macho yeyote nitakae muona ananiao ovu ya kupotosha jambo lolote la maendeleo hapa Simanjiro". Amesema Serera

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Kiria Laizer alisema kuwa wadau wa elimu na maendeleo Simanjiro wanapaswa kujitoa katika kukabiliana na upungufu wa madawati Simanjiro na Mkoa kwa ujumla kwani wanafunzi wanaosoma waweze kupata elimu bora zaidi.

"Franone wameonyesha njia nzuri katika kuisaidia jamii haaswa wanafunzi hawa wa shule ya msingi Mirerani niwapongeze sana maana kwa kujitoa kwao leo hii watoto wetu hawato teseka tena kwa swalq zima la upungufu wa madawati watasoma Kifalme kama kaulimbiu inavyo sema na mwishowe kuoitia elimu wanayo ipata itawapa nafasi ya kuwa viongozi wengine wa badae". Ameeleza Kiria Laizer.


Awali Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi Mirerani  ameeleza kuwa shue hiyo ilikwa nakabilowa na uchache wa madawati 150 kwa wanafunzi ila kwa sasa changamoto hiyo imekwisha kutokanana wadau hao ambao ni wawekezaji katika migodi ya madini ya Tanzanite ambayo ipo katika mji mdogo wa Mirerani Mkoani Manyara kujitoa kwa hali na mali ili kuondoa changamoto hiyo.


Aidha pia Mwalimu Mkuu huyo aliweza kuiomba serikali kukamilisha ujenzi wa matundo ya vyoo kwa wanafunzi ambapo kwasasa ndiyo changamoto kubwa kutokanana na shule hiyo kuwa na upungufu wa matundu 50 ya vyoo kwa wanafunzi ambapo kwa sasa ni matundu 6 tu ya vyoo ambayo yanayo tumiwa na wanafunzi wa kike huku wanafunzi wakiume wakilazimika kujisaidia shule jirani wakisubilia ujenzi buo kukamilika.













Comments