▪️ADAI SANINIU AMEKIUKA MKATABA NA KUMZURUMU MITAMBO YAKE BAADA YA KUZALISHA MADINI YALIYO MTAMBULISHA KAMA BILIONEA.
▪️AIOMBA SERIKALI KUMCHUKULIA HATUA KALI ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE.
Raia China Alia na Laizer, Auomba Ubalozi Kupeleka Kilio Serikalini Mbele ya Rais Samia ili aweze kupata haki yake.
Na Lucas Myovela, Mirerani.
Mwekezaji raia wa China, Jun Fang amepanga kuonana na Balozi wa nchi hiyo hapa nchini ili aiombe Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kumsaidia aweze kupata haki yake ambayo ni fedha na mali zake ambayo ni mitambo ya uchimbaji wa madini yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 8.5 baada ya Mbia mwenza huyo ndugu Suniniu Laizer maarufu kwa jina la Bilionea kudai anatataka kumdhurumu mali na vifaa vyake.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Mji wa Mirerani, Meneja wa Fang, Dkt Aflred Nguma alisema mwekezaji huyo mwenye asili ya China aliingia ubia ambao unamkataba na Laizer mnamo mwaka 2011 ili kushirikiana kwa pamoja kuchimba madini ya Tanzanite katika Mgodi wa Laizer uliyopo eneo la kitalu D.
Ambapo Mkataba huo ulikuwa unamtaka Mbia huyo kama mwekezaji kumiliki hisa asilimia 70 na mzawa kumiliki asilimia 30 kwa makubaliano kuwa Fang kuleta vifaa vyote vya uchimbaji vya kisasa, mtaji ,teknolojia na miundombinu pamoja na kulipa wafanyakazi wote waajiliwa wa mgodi huo.
Dkt, Nguma alisema kutokana na makubaliano hayo Laizer alikuwa na hisa ( Mgao ) asilimia 30 killa wanapo zalisha madini hiyo ni baada ya kodi zote kukatwa maana yeye ndiyo mwenye leseni ya mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Kitalu D ni mali yake lakini vifaa vyote vya uchimbaji vililetwa na mchina kupitia yeye hapa nchini katika mgodi huo pamoja na fedha taslimu za uendeshaji shughuli za uchimbaji katika mgodi huo zilikitolewa na Fang.
Alisema yeye ndio aliyemleta mwekezaji kutoka China kwani alikuwa huko katika masomo na alifanya hivyo baada ya serikali kufungua milango kwa wazawa kutafuta wawekezaji wa Nje kuja nchini kufanya uwekezaji na alifanya hivyo katika sekta ya madini.
Dkt Nguma alisema walifanya shughuli za uchimbaji kutoka mwaka 2011 hadi 2016 na kwa muda wote hakukuwa na mgogoro wowote kati ya Laizer na Fang na uzalishaji mkubwa ulifanyika na kila mmoja alikuwa akipata mgao wake na malipo halali ya kodi ya serikali yalikuwa yakilipwa bila ya matatizo.
"Mwaka 2016 mwishoni changamoto zilianza kutoka kwa Laizer na kuamua ghafla kumtafuta mtu mwingine ambae alitambulika kwa jina la Godluck Mollel maarufu kwa jina la KAKAA kuingia naye ubia wa asilimia 50 bila kumshirikisha mwekezaji wa awali ambaye ni Fang na kutaka Fang kuchukua asilimia 20 kutoka 70". Alisemaa Dkt, Nguma.
"Hata hivyo bado KAKAA alikuwa anatumia mitambo yetu na wala hatukuona shida maana tulikuwa ndani ya mkataba wa miaka 10 na tayari tulikuwa tumetumia miaka 7 na hiyo miaka mitatu amalizie Kakaa". Aliongeza Dkt Nguma.
Meneja huyo alisema mwaka 2017 hadi 2021 mgodi huo ulikuwa ukichimbwa na Mollel, Fang na Laizer na uzalishaji ukitoka mgao unakuwa tofauti na awali na hali hiyo ilifanya mwekezaji Fang kushindwa kuelewa na alipoulizwa Laizer hakuwa na majibu sahihi na kusema kuwa kitendo chake cha mahusiano serikalini kimekuwa na gharama kubwa.
Dkt Nguma alisema alifanya kila jitihada katika ofisi za madini Mirerani na Wizara ya Madini kueleza hali hiyo lakini hakuweza kupata majibu stahiki na sasa wameamua kumwomba Balozi wa China Hapa nchini ili aweze kuwasaidia kwani anaona kabisa kuna kila dalili ya yeye na Fang kudhurumiwa fedha na mali bila ya kuwa na sababu za msingi.
"Wakati Fang anaingia Ubia na Laizer mwaka 2011, Laizer hakuwa na hata sentitano ya kuendesha shughuli za uendeshaji Mgodi huo na hakuwa na hata kifaa kimoja cha kisasa kwani vifaa vyote vililetwa nchini kutoka China na mwekezaji Fang na utajiri wote alioupata Bilionea Laizer umetokana na mtaji na vifaa vilivyoetwa na mwekezaji kutoka China na Laizer anapaswa kumwogopa Mungu na kutoa vifaa vya watu na aache kusema yeye anatambulika na Serikali". Alisema Dkt, Nguma.
‘’Serikali ina nia njema na wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika uwekezaji lakini kuna wamiliki wachache wa Migodi wanaichafua sekta hiyo na kuitangaza nchi vibaya nje hivyo ni wakati wa serikali kukemea hilo na kuchukua hatua ili iwe fundisho kwa wengine’’ aliongeza Dkt Nguma
Alipotafutwa Laizer kutaka kuzungumzia suala hilo pale alipoulizwa juu ya tuhuma hizo dhidi yake zilizotolewa na Mchina Fang, Laizer hakukanusha wala kuthibitisha kwani alipoisikiliza tuhuma hiyo aliamua kukata simu na alipotafutwa zaidi mara 10 kwa siku kadhaa simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Hata hivyo jitihada zinaendelea kumtafuta Saniniu ili kuweza kujua ukweli wa jambo hilo ambapo hadi sasa Dkt, Nguma anaeleza mitambo hiyo inaendelea kubadilishwa rangi na Laizer ili kupotosha ukweli na amemtaka Laizer kujitokeza hadharani akiwa na stakabadhi za umiliki wa mitambo hiyo pindi itakapo hitajika ili tafa kujua ukweli wa sakata hilo la raia wa china.
Picha hii inaonyesha vifaa ambavyo aliagiza mchina na kuanza kufanya kazi ya uzalishaji madini katika mgodi wa Saniniu Laizer.
Comments
Post a Comment