MZIMU UNAO UTAFUNA MJI MDOGO WA MIRERANI DIWANI ASHINDWA KUUVUMILIA.

AMUOMBA RAIS SAMIA KUITIZAMA MIRERANI KWA JICHO LA UPENDO MAANA HALMASHAIRI IMESHINDWA KUWASAIDIA.

AWATAJA VIONGOZI WALIYO TOA AHADI LAKINI HADI LEO NI HEWA PAMOJA NA TAMISEMI.

Na Lucas Myovela - Mirerani.

Diwani wa kata ya Endiamtu Ndg, Luca Chimba amefunguka maziti mbele ya Mkuu wa Koa wa Manyara Mhe, Queen Sendiga na kuomba aungilie kati mmbo yanayo endekea katika Halmashauri ya Simanjiro kwa kuto zipa kipaumbele kata zinazo uzunguka mji mdogo wa Mirerani.

 

Chimba amesema kuwa wananchi walichanga fedha zao shilingi milioni 38, kipindi cha Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili kila shule iwe na maabara wanchi wa Mirerani waliitika wito huo na walichanga hadi kufanikisha kupa kiasi hicho cha fedha za kitanzania shilingi milioni 38.


Ameeleza kuwa toka mwaka 2014 hadi leo jengo halijakamilika maana wanchi walichanga na jengo likajengwa hadi kufikia hatua ya kupauliwa na sehemu iliyo bakia ilitakiwa halmashauri imalizie maabara hiyo lakini haijafanya hivyo.


"Mpaka sasa hivi shule ya Mirerani Benjamini Mkapa ndiyo shule pekee inafanya vizuri ambapo hata matokeo ya kidato cha nne 2023 / 2024 imewza kutoa divisheni 0ne 14, Two 74, Three 76, For 90 na Divisheni 0 imetoka moja tu, Na kwa kipindi cha mwaka 2023 waliyo faulu kujiunga na kidato cha tano walikuwa wanafunzi 119 pamoja na vyuo vya kati". alisrma Chimba.


"Shule inafanya vizuri lakini haina miundombinu na ikiboreshewa miundombinu itafanya vizuri zaidi ya hapo pamoja na walimu kubiresha mazingira yao ya kazi".Aliongeza Chimba.


Aidha Mhe, Chimba amesema kuwa kwa mwaka huu 2024 wanafunzi waliyo jiunga nakidato cha kwanza 540 kitu ambacho ni mzigo mkubwa kwa shule na kwa walimu, Idadi hiyo inapelekea shule hiyo kuwa na wanafunzi 1457 kitu ambacho kinaweza kupunga kupata elimu bora maana shule imeelemewa.


"Shule inaupungufu wa maabara ya sayansi katika masoma ya viumbe na binadamu ( Biology Laboratory ) tunamuomba sa Rais wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kutusaidi hili ili watoto wetu waweze kujifuza kwa vitendo haya masomo ya Sayansi". Alisema Chimba


"Vikao vya mamlaka ya mji mdogo Mirerani havijafanyika kwa zaidi ya miaka 3 vikao vya kisheria kwa madai kuwa hawana fedha zinazo toka halmashauri kuja katani". Aliongeza Chimba.

Pia chimba aliweza kumshukuru Rais kwa kuwapatia pesa na kusema kuwa Halmshauri inazibana kata zao kuzipa pesa ambayo ni kata ya Mirerani na Endiamtu hazipati fedha za mapato ya ndani na fedha zinakusanywa fenda nyingi kutoka mamlaka ya mji mdogo wa mirerani na hawapa hata sumni kwaaji ya maendeleo ya wananchi wao.


"Mfano mzuri kwa mwenyekiti wa halmashauri yetu katika kata yake ya Komoro yeye anayo madara hadi yamezidi na hayana wanafunzi cha ajabu kata ya mererrani na Endiamtu haziangaliwi na zianao watoto wengi kuliko sehemu zingine zote". Alisema Chimba.


"Mfano Shule hii ya msingi mirerani ilianzishwa mwaka 1975 na majengo yake niyatofari za udogo na hadi sasa wanafunzi wanasoma katika madarasa hayo ya udongo lakini Halmashauri yetu haioni hilo". Aliongeza Chimba.


"Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea mradi wa jengo la kisasa la Mirerani City lenye gharama ya Bilioni 5.4 ili kuendelea kuupanua mji wetu wa mirerani jengo ambalo litakuwa ni soko la masini ya Tanzanite na litaingiza fedha katika halmashauri yetu". amesema Chimba


"Jambo jingine sugu ni kituo cha Afya mirerani ambacho kina mapungufu mengi sana kinaaelemewa kwa huduma ambapo kwa siku wanaingia wagonjwa 357 ambapo nilimuomba Waziri Mkuu kukipandisha hadhi kituo hicho kuwa hosptal wakati wa kampeni 2020 na alikubali kukipandisha hadhi kuwa hosptali kamili kutokana na idadi ya watu". Aliongeza Chimba


"Tarehe 6 mwezi 6 2023 alikuja Mkurugenzi wa Afya kutoka Tamisemi Dkt Ntui, akasema katika vituo viwili vilivyo pandishwa hadhi hapa nchini ni Mirerani na Geita lakini tunashaanga hadi sasa hakuna kinacho endelea maana alisema hadi kufikia mwezi 9, 2023 majengo 12 yangeanza kujengwa ili kuleta hadhi ya kuwa hosptali lakini hadi leo hakuna kinacho endelea". alisema Chimba kwa chungu.


"Alivyo kuja Katibu Mkuu wa CCM zamani Chongolo tulimueleza na alisema tumwachie ataenda kusukuma zoezi hilo lakini hadi leo wana Mirerani hatujui kinacho endelea,Tunamuomba Rais atuangalie kwa jicho lake la huruma atuangalie ili tupate hosptali hii ambayo ni msaada mkubwa sana kwa wananchi". Alisema Chimba.

Baada kueleza hayo Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Queen Sendiga amempa siku tano Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro,Suleman Serera kuhakikisha shule ya sekondari ya kata ya Endiamtu inaanza kujengwa ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mtendaji wa Kata Mirerani,ujenzi wa Maabara na ukarabati wa majengo shule za msingi Mji wa Mirerani unafanyika haraka iwezekanavyo na sio vinginevyo.


Aidha pia Mhe  Sendiga aliweza kutoa mifuko 100 ya sementi ili kuanza ujenzi wa ofisi ya kata na kumtaka dani huyu kutoa ardhi ili ujenzi uanze mara moja na kumuagiza Mkurugenzi kupelka wataalamu wa michoro kushirikiana na diwani huyo ili kujenga ofisi hiyo ya kata.

Comments