ZAIDI YA WANAFUNZI ELFU 32 KUANZA MASOMO JIJINI ARUSHA KWA MWAKA WA MASOMO 2024.

  MAZINGIRA BORA YA UNDISHAJI KWA WANAFUNZI, WAZAZI WATAKIWA KUTO WACHELEWESHA WATOTO KUANZA MASOMO.

Na Lucas Myovela _ Arusha.


Ikiwa leo ni January 8, 2024 ambapo shule zote nchini zimefunguliwa kwaajili ya kuanza muhula mpya wa masomo kwa waafunzi wanaojinga na Sekondari, Primary na wale wa wanaoanza masomo ya Awali (chekechea ).


Kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la Arusha pekee wao wameweza kuandikisha zaidi ya wanafunzi elfu 32 wanaotarajiwa kujiunga na masomo yao katika mwaka wa masomo 2024 ambapo nikiwango kikubwa kuwai kufikiwa.

Akiongea na Mwandishi wetu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini, amesema kuwa mpaka kufikia January 6, 2024 tayari walikuwa wamesha pokea wanafunzi elfu 32 na bado zoezi lilikuwa likiendelea katika maeneo mbali mbali ya Halmashauri hiyo ya Jiji la Arusha.


"Mpaka leo January 05, 2024 wanafunzi wanao jiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika shule zetu za sekondari zilizo ndani ya Halmashauri yetu ni wanafunzi elfu kumi na nne mia nne na sabini na moja (14,471 ), Wanafunzi waliyo andikishwa kujionga na Shule za Msingi yani kuanza Darasa la kwanza ni wanafunzi elfu kumi na moja mia nne na ishirini na moja ( 11,521) na wanafu waliyo andikishwa kujiunga na masomo ya awali yani chekechea ni elfu nane mia moja sitini ( 8,160 )". Alisema Hamsini.


Akifafafanua juu ya idadi hiyo ya wanafunzi hao waliyo chaguliwa kujinga na kidato cha kwanza katika Halmashauri hiyo ya jiji la Arusha ambapo kwa idadi yao wote ni 14,471 ambapo wavulana ni 6948 na Wasichana ni 7523 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2024 katika Shule 31 za Sekondari kutwa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.


Aidha alifafanua kuwa makadilio ya wanafunzi waliyo kuwa wamekusudiwa kuandikishwa kuanza darasa la kwanza kwa mwaka 2024 ni jumla ya wanafunzi 14, 584 lakini hadi sasa wameandikisha wanafunzi 14,121 ambayo ni sawa na asilimia 78.15% ya wanafunzi waliyo andikishwa kuanza darasa la kwanza ambapo wavulana ni 5,815 na wasichana ni 5,606.


Pia ameeleza kuwa katika wanafunzi wa darasa la awali walilenga kuandikisha wanafunzi 15,191 kwa mwaka 2024 la hadi sasa wameandikisha wanafunzi 8,160 ambayo ni sawa na asilia 53.72% ya wanafunzi hao ambapo wavulana ni 4,121 na wasichana ni 4,041.


Ambapo Jumla ya wanafunzi wote waliyo andikishwa kujiunga kwa mwaka wa masomo 2024  ni Jumla ya wanafunnzi wote wa sekondari, Msingi na awali idadi yao ni 36,752.


Aidha Hamsini aliwasihi wazazi ambao bado hawaja wandikisha watoto kujiunga na masomo wafanye haraka na kwa wazazi ambao tayari wamesha wandikisha watoto wafanye mahitaji kwa wakati ili kutowachelewesha watoto katika mashomo kwa maana Jiji la Arusha linejipanga vyema katika utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi na kwawakati.


Mkurugenzi Hamsini ameeleza kuwa hadi sasa hali ya miundombinu yote kuanzia shule za msingi zipotayari kutumika kuanzia shule zitakapo funguliwa na tayari uandikishwaji wa wenye mahitaji maalum na Memkwa umekamilika kwa Mwaka wa masomo 2024.


Amesema Ufuatiliaji Katika kipindi cha kuanzia tarehe 2/01/2023 hadi 05/01/2023 jumla ya Shule za msingi 5 ambazo ni Msasani B, NAFCO, Maasai, Shangarao na Sokoni 1 ufuatiliaji umefanyika kwa lengo la kukagua ujenzi wa miundombinu unaoendelea katika shule hizo ambapo pia kupitia mradi wa BOOST; Ujenzi wa Shule mpya Msasani B umekamilika na Ujenzi wa Shule mpya NAFCO iliyopo kata ya Olmoti Miundombinu inayojengwa ni Madarasa 4 na matundu ya vyoo 11 ya ghorofa na Kazi inayoendelea ni kupanga mawe na kukusanya vifaa vya ujezi kwa ajili ya kumwaga zege.


 Pia Ujenzi wa shule Mpya Maasai iliyopo kata ya Lemara Miundombinu inayojengwa ni Madarasa 8 na vyoo matundu 22, Kazi zinazoendelea ni kusuka boksi za nguzo kwenye floor ya pili. Fundi yupo site na Kazi inaendelea pamoja na ukamilishaji wa madarasa 4 katika shule ya mdingi Murieti Darajani ambapo Kazi imekamilika, na madawati yapo na yataanza kutumika tarehe 8/1/2024.

Muonekano wa nyuma katika shule ya Sekondari ya murieti mlimani.

Muonekano wa Mbele katika shule ya Sekondari ya murieti mlimani.

Akitoa ufafanuzi kwa upande wa shule za Sekondari za Halmashauri hiyo ya Jiji la Arusha Kurugenzi Hamsini amesema maandalizi ya jumla kwaajili ya ufunguzi wa Shule kwa muhula wa masomo kwa mwaka 2024 umekamilika na shule wali zote zipo tayari kupokea wanafunzi na walimu wameshajipanga kufundisha vyema.


Ameeleza kuwa tayari wamesha tembelea Shule mbali mbali ikiwemo Kinana, Arusha Terrat, Mlimani Muriet, Moshono, Losirway, Kalimaji, Mlisho Gambo na Sekei ili kujionea miundombinu yake na hali halisi ilivyo katika maandalizi ya kupoke la wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo tarehe 8.01. 2024.


"Shule ya Sekondari Kinana ina jumla ya wanafunzi 692, kwa mwaka 2024 kwa upande wa kidato cha kwanza wanafunzi waliopangwa 236 ambapo hadi 5/01/2024 walikuwa wamechukua fomu 195 na Madawati yaliyopo ni 609 kama wanafunzi wote wataripoti kutakuwa na upungufu wa meza na viti 83 tu na Madarasa yaliyopo ni 20 yanayotumika kwa sasa ni 10 tu Madarasa 6 yamechakaa yanahitaji kubomoleewa na kujengwa upya na Madarasa 4 yanahitaji ukarabati na yanatumika". Amesema Hamsini.

"Pia Matundu ya vyoo yapo 17 kwa wasichana ambapo 12 yanahitaji uwekaji wa milango kwa sasa ipo ya bati na Matundu 12 kwa wanaume kati ya hayo matundu 4 yanatumika na matundu 8 ni mabovu hayatumiki, Pia Kuna Hosteli 2 zilizojengwa mwaka 2008 zenye uwezo wa kubeba wanafunzi 144 lakini zinahitaji ukarabati mfano rangi, kuweka Gatana milango pia Kuna Nyumba za Walimu 5 ambazo zote zinahitaji ukarabati pia Kuna jiko linalohitaji ukarabati pia". Ameongeza Hamsini.


"Katika Shule ya Sekondari Kalimaji kwa sasa wanafunzi waliopangawa ni 350,waliochukua fomu ni 130, Shule ina jumla ya vyumba 10 ambavyo 4 vinatumiwa na walimu kama ofisi, Kuna jengo la maabara 1 ambalo lilijengwa kwa mapato ya ndani kwa mwaka2021/2022, fedha iliyopelekwa ni 60 milioni na Jengo hilo linahitaji umaliziaji lakini tarehe 3/1/2024 Ceiling board kwenye veranda lilibomoka, pia chemba ya shimo limetitia kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha". Amesema Hamsini.


"Waliomba fedha nyingine ya umaliziaji Tshs 18,306,400 kutokana na hali ilivyo Mhandishi akafanye tathimini upya kwani jengo linazidi kuchakaa na Upande wa matundu ya vyoo yapo 4 kwa wavulana na 4 kwa wasichana na kuna upungufu wa matundu ya vyoo 19 kama wataripoti wanafunzi wote 350 na viti 318 kama wataripoti wote maana hii ni Shule mpyaa bado inahitaji miundo mbinu kama madarasa, jengo la utawala, maabara na Hostel". Aliongeza Hamsini.


"Katika Shule ya Sekondari Arusha Terrat wanafunzi waliopangwa 550 waliochukua fomu hadi sasa ni 371 na Jumla ya vyumba vilivyopo ni 24 kati ya hivyo madarasa 4 yamefanyiwa ukarabati kwa hiyo hakuna upungufu wa vyumba vya madarasa na Upande wa viti na meza kama wanafunzi wote wataripoti upungufu ni 350 tu". Ameeleza Hamsini.


"Hadi sasa tumepeleka Vitabu kwaajili ya Shule ya sekondari Mlimani Muriet kwa masomo yote kutoka TIE kupitia kwa RAS ambavyo ni kama ifuatavyo Biology vitabu 67,Civics vitabu 67, Chemistry 67, Geography 67, History 72, ICS Vitabu 67, Physics Vitabu 35, Baseline Vitabu 67, na Baseline kwaajili ya Walimu 53 vitabu vyote hivyo ni kwaajili ya kidato cha kwanza na Vitabu hivyo vimepelekwa tarehe 04/12/2024". Ameeleza Hamsini.

Muonekano wa vyoo vya wanafunzi katika Shule ya Muriet Darajni.

Picha; Muonekano wa wanafunzi Muriet Darajani wakiwa darasani Tayari kwa Masomo leo Tarehe 8. 01. 2024.



Comments