AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEZA UTAMADUNI WA KUSIKILIZA NA KUTATUA KWA WAKATI CHANGAMOTO ZA WANANCHI.
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, amezitaka taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza utamaduni wa kutatua kwa wakati changamoto zinazowakabili Wananchi.
Akizungumza katika zoezi la kupokea na kusikiliza changamoto za wananchi, lililofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar,amesema utaratibu huo utakuwa endelevu hadi ngazi za shehia mbali mbali mijini na vijijini.
Alibainisha kuwa kuna baadhi ya sekta za umma na ndani ya Chama Cha Mapinduzi watendaji wake wamekuwa wakishindwa kutekeleza wajibu wao na kusababisha Wananchi kuilamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika maelezo yake,Katibu huyo wa NEC Mbeto,alieleza kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kubaini na kuratibu changamoto na maoni ya Wananchi ili zitatuliwe kwa wakati na taasisi husika.
Comments
Post a Comment