RAIS DK.MWINYI AONDOA KODI YA SUKARI ZANZIBAR.

 WAFANYABIASHARA MSIPANDISHE BEI ZA VYAKULA

 Mwamdishi wetu - Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani(VAT) kwenye bidhaa ya sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo.


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe:26 Februari 2024 katika ziara yake maalumu ya alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao. 


Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewasisitiza Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar(ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.


Aidha Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itashughulikia changamoto zote za wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa bandari ya Malindi ikiwemo kufanya kazi usiku kwa kuwekewa taa na kazi kuendelea siku ya jumapili.


Akizungumza na Jumuiya ya ushirika wa Majahazi na Wafanyabiashara katika bandari ya Malindi pia amezungumza na Wafanyabiashara wa soko kuu la Darajani katika mwendelezo wa ziara yake maalumu ya kutembelea masoko na kusikiliza changamoto zao Mkoa wa Mjini tarehe: 26 Februari 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula katika kuwahurumia na kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan .


Rais Dk.Mwinyi ametoa maagizo kwa Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (ZEEA) kuwapatia mikopo wafanyabiashara walio kwenye maeneo maalumu ya biashara. 


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewataka viongozi wa Manispaa, Wilaya, Mkoa kuwapanga Wafanyabiashara kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao.

Comments