WADAU ZAIDI YA 1000 KUSHIRIKI, WAKIWEMO WAFANYABIASHARA, MABALOZI, SEKTA BINAFSI ZA NDANI NA NJE YA NCHI.
Na Lucas Myovela - Arusha.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua jukwaa la kodi na uwekezaji la mwaka huu, lililoandaliwa na Wizara ya fedha kwa lengo kusaidia kuandaa bajeti ya mwaka 2024/2025.
Hayo yalisemwa Jijini Arusha na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya na kuongeza kuwa kongamano hilo ni utaratibu wa kawaida ambao unawahusisha wananchi na wadau wengi kupitia utoaji wa maoni yao.
Alisema jukwaa hilo litafanyika Jijjni Dar es salaam na kushirikisha wadau 1000 wakiwemo wafanyabiashara,mabalozi, wadau sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi.
"Baadhi ya malengo ya jukwaa hili ni kuangalia mustakabali wa ulipaji wa kodi,hali ya uchumi na uchumi jumuishi,kuangalia wafanyabiashara wanaoanza biashara, ili kuwawezesha biashara zao kukua". Alisema Mwandumbya.
Kwamujibu wa Elijah, tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo, wamepata mafanikio mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato, ambapo kwa kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana, serikali imekusanya mapato kwa asilimia 12, bapo kwa kipindi cha Disemba pekee walikusanya Trilioni tatu.
Alisema licha ya hayo mafanikio, bado kuna changamoto mpya zinazojitokeza na wanazitafutia suluhisho, kwa wakati ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya kuongeza na kuchochea ufanisi.
Pia alisema wameongeza uahindani kwa kuwasajili wafanyabiashara wenye mitaji ya sh,milioni 200, kwenye mfumo wa ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Kuna haja ya kufanya Tafsiri upya kwenye Sheria za Kodi Nchini Tanzania. 1.Tafsiri ya VAT na 2. Mkusanya Kodi na Mtoza Kodi. 3. Mtaji wa Biashara na Mauzo ya Biashara. Hapa Kuna taarifa za Msingi zilisha kiukwa, ndiyo Maana Changamoto ya Kodi Nchini kwetu inapotezwa
ReplyDelete