TAFITI ZIMESAIDIA KUPATA SERA NA MTAALA MPYA WA ELIMU WENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA.

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA TAASISI YA NELSON MANDELA KWA MAPINDUZI MAKUBWA YA KISAYANSI.

Na Lucas Myovela, Arusha.

Kamati ya Kudumu ya Bunge, Elimu, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetembelea Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwaajili ya kujionea mradi wa ujenzi wa mabweni kwa wanachuo unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 16.28 hadi kukamilika kwake.

Mradi huo wa mabweni ambapo ukikamilika utatatua changamoto ya uhaba wa mabweni kwa wanachuo hususani wakike wanaofika kusoma na kufanya tafiti mbalimbali zenye matokeo chanya kwa wananchi zikiwemo tafiti za kilimo sanjari na sekta nyingine za kuinua uchumi wa kati kwa taifa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe, Hussna Sekiboko (Mbunge) alisema kuwa wamelidhishwa na maendeleo ya mradi huo na kuitaka serikali iweze kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliyo pangwa ili wanafunzi wanaofika chuoni hapo hasa wakike ambao wanafamilia waweze kupata makazi mazuri ambayo yatamuwezasha kufanya tatifiti zake kwa uhuru.


"Tumeridhishwa na mradi huu kikibwa tunaiomba serikali iweze kuangalia kwa ukaribu taasisi hii ya Nelson Mandela maana ni kiunganishi kikubwa katika mageuzi ya kisayansi kutokana na tafiti zinazo fanyika katika taasisi hii, na mabweni haya yakikamilika yatakuwa yamerahisisha sana miundombinu kwa wanafunzi wakike ambao wenda wanafamilia zao na wameamua kujiendelea kujiendeleza katika nyanja hii ya sayansi". Amesema Mhe, Sekiboko.

"Serikali inatoa fedha ili miradi hii iendelee na iweze kutoa matokeo chanya kwa watanzania na mradi huu unatekelezwa kwa bajeti ya mwaka 2023 & 2024, Mradi huu ni mkubwa kama mnavyo fahamu chuo hiki ni cha kimataifa kichukua wanaguzi pamoja na wahadhiribwa ndani ya nchi na nje ya nci kwa hiyo lazima bajeti yake iwe kubwa na serikali iajitahidi kwa asilimia kubwa kufanikisha hilo". Ameongeza Sekiboko.


Aidha Mhe, Sekondo ameeleza kuwa fedha ambazo serikali ilitenga kwa mwaka wa fedha uliyo pita tayari zote zimeshalipwa na zipo site zinafanya kazi na wao kama kamati wataenda kushawishi serikali kuongeza fedha zaidi kwa mwaka huu ili iweze kutolewa na kukamikisha mradi huo kwa haraka.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga aliishukuru kamati hiyo kuweza kutembelea ujenzi huo wa mabweni uliotengewa fedha kwa mwaka wa gedha 2023/24 ambapo mabweni hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 500 kwa wakati mmoja.


"Mradi huu ulianza mwaka 2021/22 ingawa maendeleo si mazuri sana na ulipaswa ukamilike ndani ya miaka miwili na mradi ulisimama kutokana na fedha zilizokuwa zimetengwa kuchelewa kutoka na hadi kufikia leo hii mradi huu upo 65% na tumepokea maagizo ya kamati na sisi kama wizara tunaenda na hili na kulipa kipaumbele jambo hili katika bajeti zetu maana taasisi hii ni kubwa na tutajitahidi mradi huu uweze kukamilika kwa haraka". Amesema Kipanga.

"Katika mabweni haya kutakuwa na vyumba maalamu vitakavyo wasaidia wafanzi wa kike wanaokuja na watoto na wasaidizi wao wa kazi, Lengo kuu na kuweka vyumba hivi ni kuweka chachu kwa wanafunzi wengi wa kike kuendelea kusoma masomo ya sayansi". Aliongeza Kipanga.


Aidha Mhe, Kipanga ameeleza kuwa katika mageuzi na mabadiliko ya ukuaji wa elimu yametokana hasa na tafiti mbali mbali zinazo fanywa hadi kupata sera na mitaala mipya ya elemu kwa wanafunzi ambay tumeanza kuitekeleza katika mwaka wa masomo 2024.

"Bila tafiti tusingeweza kubadili sera yetu ya elimu, tuliweza kufanya tafiti kama serikali na tulibaini masuala mbalimbali na yale yaliyokuwa na mapungufu tukafanya maboresho na sasa tumekuja na mtaala unakwenda kujibu na kutatua changamoto za jamii pamoja na ubora wa elimu katika nchi yetu na kufanya kiwango cha elimu yetu kuwa wa kiwango cha kimataifa". Alisema Kipanga.


Awali Makamu Mkuu wa Chuo cha (NM-AIST) Profesa, Maulililo Kipanyula, akiongea mbele ya kamati hiyo amesema hatua mbalimbimbali za ujenzi wa mabweni hayo ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 500 kwa wakati mmoja yakuwa chachu kubwa kwa wanafunzi wanao jiunga na taaasisi hiyo.


Profesa Kipanyula alisema mradi huo wa mabweni pacha matatu unatekelezwa kwa kiasi cha shilingi Bilioni 16.28 ambapo yakikamilika mabweni hayo yatatoa kipaumbele kwa wanafunzi wakike wanaokuja na familia zao.

"Ujenzi huu unatekelezwa kwa awamu tatu lengo ni kuongeza fursa kwa wanawake katika kushiriki katika masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu na mpango wa ujenzi huo ni wa miaka mitano na kila awamu itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.8 awamu ya kwanza na lengo la mradi huu ni kutengeneza fursa kwa wanawake naujenzi wa hosteli hiyo imefikia asilimia 49". Ameeleza Kapanyula.

"Mabweni haya yapo katika mfumo wa apatimenti zenye vyumba viwili vinavyomuwezesha mwanamke anaye nyonyesha kupata nafasi ya kusoma na kuishi na familia yake lakini pia kutoa nafasi zaidi kwa wanawake kupenda zaidi masomo ya sayansi na mwaka ujao wa fedha watakamilisha ujenzi huo kwa asilimia 100". Ameongeza Kapanyula.



Pia kamati hiyo iliweza kujione tafiti mbali mbali zinazo fanywa katika taasisi hiyo ya Sayansi ikiwemo mradi mkubwa na wakisasa wa kompyuta ijulikanayo kama "Param Kilimanjaro " yenye uwezo wa kuchakata data kwa kasi na kuzihifadhi kutoka taasisi mbalimbali za serikali ambapo mtambo huo unasadikika kuwa wakipekee katika nchi za Afrika Masharika na kati.


Aidha kamati hiyo pia iliweza kushuhudia studio za kisasa za kufundishia wanafunzi popote walipo duniani kwa njia video, Pia taasisi hiyo iko mbioni kufungua kituo cha Radio ili kuendelea kutia mafunzo ya kitafiti kwa wananchi ili waweze kunufaika na taasisi hiyo.




🔴PICHA ZA UJENZI MRADI WA MABWENI UNAO GHARIMU SHILINGI BILIONI 16. 28 HADI KUKAMILIKA KWAKE AMBAO UNATEKELEZWA KWA AWAMU TATU KATIKA TAASISI YA SAYANSI YA NELSON MANDELA.






🔴MRADI WA MABWENI UTAKAPO KAMILIKA UTAKUWA HIVI.





🔴PICHA MBALI MBALI ZA MATUKIO.















Comments