BREAKING NEWS: SAFU MPYA YA DKT SAMIA NDANI YA CCM, MONGELLA NAIBU KATIBU MKUU, MAKALLA MRITHI WA MAKONDA.
ALLY HAPI, ARUDI KWENYE MFUMO WA CHAMA, JOKATE NAE APELEKWA KWA VIJANA UVCCM.
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo April 03, 2024 Jijini Dar es salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine imemchagua Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Ndug Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo April 03, 2024 Jijini Dar es salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine imemchagua Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, akichukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo April 03, 2024 Jijini Dar es salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine imemchagua Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akichukua nafasi ya Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan , akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokutana leo Jumatano, Aprili 2024, jijini Dar Es Salaam.
Comments
Post a Comment