WAMUOMBA WAZIRI KUCHUNGUZA KIUNDANI, WANADAI KUTISHIWA KWA KUWATAJA WAKUBWA SERIKALINI.
Na Lucas Myovela, Mirerani
WAMILIKI wa migodi ya madini ya Tanzanite iliyopo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamemwomba Waziri wa Madini hapa nchini, Antony Mvunde kuwa macho na Wataalamu Waangalizi wa serikali migodini maarufu kwa "Majicho serikali", kutoka Wizarani waliyopelekwa kwenye machimbo hayo kwa madai kuwa wako kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe na kufanya serikali kupoteza mamilioni ya fedha za kodi katika tathimini ya madini hayo.
Mmoja wa wamiliki wa mgodi wa madini ya Tanzanite ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake alisema pamoja na kupeleka malalamiko kwa Afisa Madini Mfawidhi Mirerani Bw, Nchahwa Chacha, kuwa hadi sasa hakuna majibu yeyote na wameamua kumwandikia barua Waziri Mvunde juu ya hali hiyo inayoendelea katika machimbo hayo ya Mirerani.
Mmiliki huyo alisema waangalizi hao wa serikali mara baada ya mgodi kutoa uzalishaji wa madini ya Tanzanite huja katika mgodi kwa ajili ya kuangalia uzalishaji huo na kuzama mgodini na kuanza kupora madini na kuyaficha na yanayopelekwa kwenda kwenye tathimni ni madini machache na yasiyokuwa na thamani na serikali kukosa mapato kwani madini mazuri yamechukuliwa na watalaamu hao biloa ridhaa ya mmiliki wa mgodi.
Alisema hali hiyo imekuwa kero kwa wamiliki wa migodi na kufikia hatua kufikisha malalamiko kwa Afisa Madini Mfawidhi Mirerani lakini hakuna hatua yeyote hadi sasa inayochukuliwa na kufikia hatua wamiliki hao kujenga chuki na watalaamu maana wanatumia rasilimali fedha nyingi katika uchimbaji wa madini hayo na kuwanufaisha wengine wasiyo jua upatikanaji wake.
Mmiliki mwingine yeye alitoa lawama zote kwa Afisa Madini Mfawidhi Mirerani, Nchahwa Chacha kwa kuwa kimya bila kuchukua hatua pamoja na kupewa taarifa hiyo na ndio maana wamemwomba Waziri Mavunde afuatilie hilo na ikiwezekana achukue hatua dhidi ya wahujumu wa Serikali katika mapato.
"Chacha anajua kila kitu na kuna mmoja wa wataalamu hao ni ndugu na kigogo Wizara ya Madini amekuwa na kauli ya jeuri kwa wamiliki wa migodi kwani amekuwa akijinasibu kuwa nyie chongeeni lakini sisi tumekuja kikazi". alisema mmoja wa wamiliki wa mgodi.
"Wamekuwa wakija migodini kwa nia ya uhakiki cha kushangaza wanachuka baadhi ya madini na kusema haya niya wakuu sasa na hatujuibyanatokaje na wanafanyia uthamishaji wapi kwakweli hii mekuwa ikituumiza kweli maana wanaweza chukua madini yenye thamani kubwa na kukuachia ya kaida yasiyo na thamani kubwa, Sasa tunata kujua hao wakuu ni wakina nani wanao tuma hawa majicho kuchukua madini yetu". Aliongeza Mmiliki huyo wa Mgodi.
Mfanyabiashara mwingine wa Tanzanite Mirerani alisema kuwa Wizara ya Madini kila mtumishi katika sekta hiyo anasharubu kama "kambare" na wanapoagizwa na serikali kwenda Mirerani kusimamia udhibiti utoroshaji madini na kufanya tathimni sahihi kwa kile kilichopatikana kwa faida ya serikali hiyo inakuwa toufati na kuanza kujitajilisha wao na kuifanya serikali kukosa mapato hatua ambayo wafanyabiashara wanasingiziwa kutorosha madini nje ya nchi kitu ambacho sio kweli.
Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu ya kiganjani, Afisa Madini Mfawidhi Mirerani Nchahwa Chacha, alisema hana taarifa rasmi za malalamiko hayo na kusema kuwa Mji wa Mirerani ni mji wa maneno mengi sana na hivyo hawezi kufanyia kazi porojo za mtaani kwani sio utaratibu wa kiserikali.
Chacha alikiri kuwepo kwa wataalamu hao ndani ya ukuta wa migodi ya Tanzanite wenye lengo moja tu la kusimamia uzalishaji na kufanya tathimini sahihi kwenye mgodi unazalishaji madini na sio vinginevyo.
Alisema yeye kama msimamizi Mkuu wa Migodi hiyo toka Wizara ya Madini hana taarifa rasmi na kama yapo basi hayajamfikia ofisni kwake na aliwataka wamiliki wa mogidi ya Tanzanite kufikisha malalamiko rasmi ofisini kwake ili yaweze kufanyiwa kazi na ikibidi hatua stahiki zichukuliwa ikibainika hivyo.
Awali tulimpata Katibu Mkuu na kumueleza sakata hilo na kueleza kuwa ni vyema jambo hilo akatafutwa Waziri mwenyewe ndiyo alitolee ufaanuzi, hadi habari hii inaenda hewani bado tunamtafuta Waziri wa Madini ili atolee ufafanuzi jambo hilo ambalo linaonekana kuwa mwimba kwa wachimbaji hao.
Jitihada za makusudi ziliendelea kufanyika kumtafuta Waziri wa Madini Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw, Kheri Mahimbali ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo za wachimbaji madini ya Tanzanite dhidi ya Majicho ya Serikali.
Mwisho.
Comments
Post a Comment