WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUTAFUTA ENEO JINGINE KUJENGA OFISI YA KATA KUTOKANA NA MAFURIKO YA MARA KWA MARA.

SHUGHULI ZOTE ZA OFISI YA MTENFAJI ZIMEAMIA SHULENI.

Na Lucas Myovela - Arusha

Picha; Ofisi ya Kata ya Moshono ikiwa imejaa maji mara baara ya vua zinazo endelea kunyesha Jijini Arusha ambapo kwasasa imefungwa na Shughuli zote za kiserikali zimehamishiwa Shule ya Msingi Moshono.


Wananchi wa Kata ya Moshono Jijini Arusha wameieleza Motive Media kuwa Jitihada za ziada zinahitajika kupata eneo lingine la ujenzi wa ofisi ya kata ya Moshono iliyopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha baada ya ofisi hiyo ya kata kuingia maji kila mvua kubwa inaponyesha.


Mmoja wa wakazi wa kata ya Moshono aliyejitambulisha kwa jina la Lodvick Mollel alisema inasikitisha sana kuona watendaji wa kata ya Moshono wamekuwa kama wakimbizi pindi mvua inaponyesha kwani ofisi hiyo ilijengwa eneo la Tindiga.


Mollel alisema kwanza hatua ya ujenzi wa ofisi ya kata ya Moshono katika eneo la Tindiga ni kosa na kiufundi inasikitisha kuona injinia wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuruhusu ujenzi katika eneo hilo lenye unyevunyevu wakati wote wa mwaka na kutumia mamilioni ya pesa.


Alisema hakuna jinsi lazima ofisi ya kata ya Moshono iondolewa katika eneo hilo ili kuwapa nafasi watendaji wa kata wa idara zote kufanya kazi kwa uhuru bila kusumbuliwa.


Naye Jovina Massawe mkazi wa mtaa wa Moshono Kati ndani ya kata ya Moshono alionyesha kusikitishwa na ofisi ya kata kuwa katikati ya dimbwi kubwa la maji na hakuna jinsi ya kuingia ofisini hatua ambayo huenda ikaleta madhara makubwa ya magonjwa ya kuambukiza.


Massawe aliosema jitihada za ziada zinahitajika Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Juma Hamsini kutafuta eneo lingine kwa ajili ya ujenzi wa ofisi kwa ilipo ofisi hiyo sio sehemu Rafiki.

Diwani wa Kata ya Moshono,Maryam Kissawike alipoulizwa juu ya ofisi hiyo ya kata kujaa maji ndani ya nje alionyesha kusikitishwa na kusema kuwa hiyo inaleta usumbufu kwa wananchi wa kata hiyo kupata huduma katika ofisi hiyo ya serikali lakini kwa sasa imehamia shule ya Msingi Moshono kwa dharura.


Kissawike alisema hana pingamizi na ofisi kuhama eneo hilo ila alishauri ujenzi wa kisasa katika eneo hilo lenye tindiga kwani ofisi nyingi na viwanja vya mpira wa miguu hujengwa katika maeneo ya tindiga kinachopaswa kuzingatia ujenzi huo wapewe wenye sifa.


Alisema kwa sasa ofisi ya kata ya Moshono imehamia kwa muda katika chumba kimoja katika shule ya Msingi Moshono na kufanya huduma zote kama vile elimu,afya,biashara hatua ambayo sio salama kiutendaji na kiusalama kwa nyaraka za serikali.

Mtendaji wa Kata ya Moshono,Anna Lebisa alikiri kuhama ofisi na kuhifadhiwa katika shule ya Msingi Moshono na kusema kuwa wanatarajia kuwasilisha ombi kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi eneo jingine.


Alisema pamoja na ufinyu wa eneo walilohifadhiwa shule hawana jinsi kwani ofisi ya zamani imezingirwa maji ndani na nje na hiyo hutokea pindi mvua kubwa inaposhesha na wao hufanya kazi katika mzingira magumu na wananchi wengi kukosa huduma kwa kutojua ofisi zilipo.


Mtendaji alisema jitihada za ziada zinahitajika ili ipatikane eneo jingine kwa ajili ya ujenzi wa ofisi lakini sehemu ilipo zamani ofisi ya Kata ya Moshono sio salama kiafya na kihuduma kwa pande za wananchi na watendaji wa kata.


Mwisho.

Comments