RC MAKONDA AMBANANISHA MENEJA WA RUWASA LONGIDO, ATHIBITISHA KUMTOMUHITAJI WILAYANI HAPO KUTOKANA NA UONGO PAMOJA NA UZEMBE WA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAJI.
Ikiwa ni mwanzo wa ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda aliyoipa jina la SIKU 6 ZA MOTO ARUSHA.
RC Makonda Ametembelea katika Zahanati ya kijiji cha Leremeta Wilayani Longido ambapo akiwa hapo amepokea malalamiko kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Leremeta Bw. Supuk Melita na Wananchi wakazi wa eneo hilo kwa ujumla kuwa kulikuwa na mradi wa maji wa Tsh Milioni 210 lakini zilitolewa fedha Tsh Milioni 150 na hadi sasa mradi huo haujakamilika na kuna zaidi ya miezi 6 hakuna kinachoendelea.
Mara baada ya kusikiliza malalamiko ya Wanachi wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa serikali ya kijiji Bw.Melita, RC Makonda alimtaka Meneja RUWASA Wilaya ya Longido Mhandisi. Ramadhani Musiba, kutolea majibu na kumuhoji ni lini amefika kukagua muendelezo wa mradi huo.
Naye, Mhandisi. Ramadhani alianza kwa kumuaminisha RC Makonda kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu wa 2024 mradi huo utakuwa umekamilika, majibu ambayo bado hayakutosheleza kwakuwa mradi huo umesimama kwa zaidi ya miezi 6.
Kutokana na kutoridhishwa kwa majibu hayo, RC Makonda alimuhoji tena Mhandisi. Ramadhani amueleze ni lini mara yake ya mwisho kutembelea mradi huo katika kuhakikisha anaondoa adha ya kiu ya maji kwa wananchi wakazi wa eneo hilo na zahanati hiyo ya Leremeta kupata maji safi na salama.
Naye, Mhandisi. Ramadhani aliendelea kuonesha hali ya uongo kwa kutoa majibu ambayo yalikataliwa na uongozi wa kijiji hiko na wananchi kwa ujumla na hatimaye alipobananishwa kueleza hali halisi iliyopo hadi sasa ili kuhakikisha zahanati ya Leremeta inapata maji safi na salama na kijiji kwa ujumla, akajikuta anakosa majibu ya uhakika.
Kutokana na hayo yote, RC Makonda hakusita kumwambia ukweli Meneja huyo wa RUWASA wilayani Longido ya kuwa ameshindwa kufanya majukumu yake ipasavyo na kumwambia kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa haridhishwi na hataki aina ya watumishi kama yeye wenye uzembe katika usimamizi wa miradi na majibu ya uongo.
" Ndani ya mkoa wetu wa Arusha, nataka mtu anayethamini kazi aliyopewa, kulinda miradi ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, sasa mwambie leo hii Katibu Mkuu wizara kuwa Mhe. RC hanitaki pale Arusha kwasababu ya uongo wangu na uzembe wa kutofuatilia kwa ukaribu miradi ya maji Longido". Amesema Rc Makonda.
Comments
Post a Comment