WAWILI WABAINIKA KATIKA SAKATA ZITO LA KUGUSHI NYARAKA FEKI ZA MLIPA KODI NA KAMPUNI HEWA KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA.

 TAKUKURU YASEMA MUDA WOWOTE KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MUJIBU WA SHERIA.

Na Luas Myovela - Arusha.


Tuhuma nzito za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma zimechukua sura mpya baada ya watumishi wawili kudaiwa kuhusika kutengeneza namba bandia ya mlipakodi na kampuni hewa ya kulipia makusanyo hayo.


Kutokana na uchunguzi huo wa awali kubainisha hilo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, imefanya uchunguzi wa mfumo mzima wa malipo ili kubaini makampuni mengine hewa na namba bandia za mlipakodi zilizotumika kuchepusha kodi au mapato yoyote katika halmashauri ya Jiji la Arusha.

Zawadi Ngailo, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha.

Akiongea na Motive Tv Mapema leo Mei 27, 2024 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo amesema uchunguzi wa awali umebaini watumishi wawili wa halmashauri hiyo wamehusika kughushi nyaraka ikiwamo kutengeneza namba bandia ya mlipakodi na kutumia kampuni hewa kulipia mapato.


Ngailo ameeleza kuwa kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, tayari taasisi hiyo ilikuwa imesha anza uchunguzi wao wa awali toka siku ya kwanza walipo pata malalamiko hayo.


"Maelekezo yalitolewa kwenye kikao kati ya Mkuu wa Mkoa na wafanya biashara wa utalii Mkoani Arusha na ofisi ilikuwa imeshaanza uchunguzi na uchunguzi huo ulikuwa unahisisha idara ya mapato ( Ushuru wa Huduma ) katika Halmashauri ya Jiji la Arusha". Ameeleza Kamanda Ngailo.


" Kwa hiyo hadi sasa uchunguzi umefikia hapo ambapo tumeweza kuwabaini watu wawili kutokana na uchunguzi tuliyo ufanya na kuwabaini hao watuhumiwa, inamaanisha tulihoji watu ambao ni mashahidi na pia tuliwahoji na watuhumiwa wenyenye na tuliweza kuwabaini hao watu wawili lakini bado uchunguzi unaendelea". Aliongeza Ngailo.


Aidha kamanda huyo wa Takukuru ameeleza kuwa katika uchunguzi huo waliyo ufanya na wanaoendelea kuufanya utakapo kamilika hatua itakayo fuata ni kuwafikisha mahakani watuhumiwa wote waliyo husika na ubadhilifu huo wa mamilioni ya fedha.


"Hatua inayofuata tutakapo kamilisha tutawafikisha mahakamani kwa mujibu wa utaratibu na uchunguzi huu unahusisha wale wote waliyokuwa wanahusika na ukusanyaji wa mapato (Ushuu wa Huduma) na lengo la kuchungua ni kuhakikisha wote tulio wabaini wanafikishwa mahakamani". Amesema Ngailo.


Ikumbukwe Takukuru inafanya uchunguzi huo ikiwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kufuatia tuhuma zilizowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato), Wilbard Chambulo kudai kulipa kodi ya huduma Shilingi milioni 24, lakinilakini akapewa risiti ya Shilingi milioni 3.6 kitu ambacho ni tofauti na mfanyabiashara huyo alicho kilipa.


Hata hivyo taarifa fiche zimebaini kuwa makampuni hayo feki yalitengenezwa miezi ya mwishoni mwaka 2022 kitu ambacho Mkuugenzi wa hivi sasa Juma Hamsini hakuwepo na hakuwa Mkurgenzi wa Jiji la Arusha ijapokuwa watumishi hao walikuwepo katika kitengo hicho.

Pia kufuatia malalamiko ya mfanyabiashara huyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini alitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habaei juu ya kile alichokuwa anakijua na alicho kikita ofisini kwake kitu ambacho kiliibua mambo mapya hadi kupelekea Rc Makonda kutoa tamko la kufanyika uchunguzi huo kwa kupitia Tasisi ya Kupambana na rushwa Takukuru.

Aidha ikumbukwe  Juni 13, 2023 Juma Hamsini alikabidhi rasmi Ofisi na kuwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo ya Jiji la Arusha baada ya kuteuliwa mnamo tarehe 07 Juni , 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Motive Media Tanzania inaendelea kufuatilia kwa karibu sakata hili ili kuweza kubaini kiundani zaidi juu ya sakata hili la ubadhilifu wa fedha na kukuletea majina ya wote waliyohusika pindi watakapo ikishwa mahakamani kama alivyo eleza Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha Zawadi Ngailo.

Comments