![]() |
Na Lucas Myovela - Arusha. |
MAFANIKIO MAKUBWA YAPIGWA NA SHIRIKA LA POSTA KUTOKA WATANZANIA KUANDIKA BARUA KWA MKONO HADI KUTUMIA NJIA YA KIDIGITALI.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Mzee Suleiman Mndewa amelitaka Baraza la Wataalamu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kuhakikisha linakwenda na wakati katika utendaji kazi wake kwani teknolijia ya mtandao inakuwa kwa kasi hivyo na wao wanapaswa kujipanga kukabiliana na changamoto hiyo kiutendaji.
Mndewa alisema hayo June 03, 2024 wakati akifungua Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ambapo Nchi 46 wanachama wa umoja huo walishiriki na Mkutano huo ulifanyikja Makao makuu ya Umoja huo Jijini Arusha.
Alisema Dunia ya sasa inakwenda kwa kasi sana katika suala la teknojia mtandao hivyo watalaamu wa PAPU nao wanapaswa kujipanga na kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili kuwahakikishia wateja wao huduma bora na ya kisasa.
Naibu Huyo alisema bado nchi nyingi za Afrika zina changamoto ya miundombinu hivyo ni wakati wa wataalamu wa PAPU kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili kuja na mapango kazi wenye tija kwa nchi hizo ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na teknojia mtandao ya kisasa.
Alisema ni wakati wa Wataalamu wa PAPU kuangalia changamoto za kimawasiliano na kuzitafutia ufumbuzi kwani hiyo ndio njia pekee ya kutaka umoja huo kwenda na wakati katika utendaji kazi wa kila siku.
"Dunia inakwenda kasi katika suala la teknolojia mtandao hivyo ni wakati wa PAPU kujipanga na kukabilianana hali hiyo ili umoja huo uweze kuendesha shughuli zake kisasa tofauti na zamani’’. alisema Mndewa.
Naye Katibu Mkuu wa PAPU ,Dkt Sifundo Chief Moyo alisema katika kikao hicho cha wataalamu wa umoja huo watahakikisha wanajadili kwa kina namna bora za kiutendaji za teknolojia mtandao kwa nchi zote wanachama wa umoja huo ili ziweze kufanya kazi kisasa tofauti na zamani.
Alisema ni wakati wa umoja wa PAPU kuungana na kushirikiana pamoja na kujadili kwa kina changamoto zote za kiwamasiliano na kuja na mpango kazi wenye tija na kutaka umoja huo kufanya kazi kisasa ili umoja huo uende sambamba na teknolojia inayokuwa siku hadi Duniani.
Kwa upamde wake Posta Master Mkuu Shilrika la Posta Tanzania Ndg, Maharage Chande alisema kuwa Shirika la Posta Nchini linapasa kujipanga kikamilifu na kutoka katika utendaji kazi wa kizamani na kwenda kisasa kwani teknlojia inakuwa siku hadi siku.
Chande alisema zamani wananchi walikuwa wakiandika barua katika kuwasiliana na kulitumia shirika hilo katika kusafirisha barua lakini sasa jamii hiyo haifanyi hivyo,hivyo basi ni wakati shirika hilo kubadilika na kutafuta namna bora ya kimawasiliano katika kuwasiliana ili kwenda na teknolojia ya kisasa inavyotaka ikiwa ni pamoja na kutafuta namna bora na ya haraka ya kumuhudumia mwananchi.
"Sekta ya Posta bado inamchangomkubwa katika Uchumi na maendeleokwa kuzingatia masuala ya utawalaikiwemo ajenda ya Kupokea na kufanyiakazi matumizi ya akili mnembayaani(Artificialintelligence). Katika hali hiyo ipo haja kwa mataifa haya kuzidi kuimarisha shughuli za kibiashara ili kukuza uchumi wa mataifa haya pamoja na ulipaji Kodi" Alisema Postamasta Mkuu Maharage Chande.
Mkutano huo wa 42 wa Baraza la Utawala Afrika umewakutanisha Wataalamu mbalimbali kutoka mataifa zaidi ya 15, sambamba na ufunguzi wa Vikao vya Wataalamu wa masuala ya Posta kwa maendeleo ya mataifa hayo yanayo unda umoja wa Posta barani Afrika.
Comments
Post a Comment