UKUAJI MKUBWA SEKTA YA AFYA NA UJENZI WA OPD COMPLEX KATIKA HOSPTALI YA ARUSHA CHINI YA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN NA USIMAMIZI BORA WA MKURUGENZI JUMA HAMSINI KATIKA MAPINDUZI YA SEKTA YA AFYA JIJI LA ARUHA.
NI MAKALA MAALUM INAYO ANGAZIA MABADILIKO SEKTA YA AFYA NA UJENZI WA OPD COMPLEX KATIKA HOSPTALI YA JIJI LA ARUSHA, IMEANDALIWA NA LUCAS MYOVELA.
Leo tunaangazia Ujenzi wa Jengo kubwa la OPD COMPLEX katika hosptali ya Jiji la Arusha ambayo ni alama kubwa ya ukuaji mkubwa na utoaji huduma kwa jamii katika Sekta ya Afya hapa nchini chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika bajeti ya Afya ya mwaka wa fedha 2024 / 2025, Rais Dkt. Samia kupitia Wizara ya Afya ameipa kipaumbele kikubwa ili kuboresha Sekta ya Afya lengo likiwa ni kutoa huduma bora za kitabibu kwa watanzania wote hapa nchini.
Mnamo tarehe 13 May 2024, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliadhia kwa pamoja na kupitisha Bajeti ya Wizara ya Afya ya jumla ya Shilingi Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Tatu Kumi na Moja, Milioni Mia Nane Thelathini na Saba, laki Nne na Sitina na Sita elfu (1,311,837,466,000.00) ili kuweza kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Mradi wa ujenzi wa jengo la OPD Complex ulianza tarehe 01/03/2022 ambapo mradi huu ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji miundombinu ya afya na kusogeza huduma karibu kwa wananchi katika jiji la Arusha na maeneo jirani ya Jiji hilo.
Awali Mradi huo ulianza kutekelezwa na Mkandarasi B.H.LADWA ukiwa chini ya MHANDISI MSHAURI (CONSULTANT): SANSUTWA SIMTALI LIMITED, ambapo kwa awamu ya kwanza ni ujenzi wa sakafu ya Chini ya Jengo la OPD Complex.
Aidha kutokana na Mkandarasi huyo kuonyesha hali ya kusuasua katika utekekezaji huo wa mradi mnamo tarehe 15/08/2023 Mkandarasi huyo alisitishiwa Mkataba wae na kwa sasa Mradi huu unatekelezwa na Jiji la Arusha kwa njia ya “Force Account”.
Hata hivyo hadi hivi sasa Gharama zilizotumika kwa malipo ya Mkandarasi katika ujenzi huo ni Jumla ya ShilingiBilioni moja,Milioni mia sita hamsini na tano,elfumbili mia mbili tisini na nane (1,655,002,298.00) ambapo fedha za Serikali kuu ni Shilingi Bilioni Moja (1,000,000,000) na Mapato ya Ndani yakiwa ni Shilingi Milioni mia sita hamsini na tano (655,000,000.00.).
Aidha katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la OPD COMPLEX katika hosptali ya Jiji la Arusha unaoendelea katika Kata ya Engutoto mradi huo kwasasa umefikia asilimia 85% ya utekelezajivwake.
Ambapo lengo kuu la Mradi huo mkubwa kutekelezwa katika Jiji la Arusha ni Kuongeza miundo mbinu ya Hospitali ya Jiji ili kuboresha utoaji huduma za afya katika halmashauri ya jiji la Arusha.
Ujenzi wa Jengo hilo litakapo kamilika litakuwa na sakafu mbili,ambapo ni sakafu ya chini, sakafu ya kwanza, na sakafu ya pili na kiila sakafu imesanifiwa kuwa na idara nne, hivyo hospitali hiyo itakuwa na idara kumi na mbili itakapokamilika.
Katika Sakafu ya Chini itakuwa na idara ya Ushauri wa kidaktari na usafishaji damu (Consultations and Dialysis), Idara ya Dharura (Emergency department), Idara ya mionzi (Radiology), ambayo ni huduma za X-rays, Magnetic Resonance imaging (MRI), Ultrasound, CT scan na Fluoroscopy (Huduma ya Uchunguzi wa Mwili Mzima) pomoja na Idara ya Madawa (Pharmacy).
Pia katika Sakafu ya kwanza itakuwa idara ya watoto RCH, Idara ya Maabara, Idara cha Meno pamoja na idara ya Macho na Masikio.
Aidha pia katika Sakafu ya pili itakuwa na idara ya uangalizi maalumu (ICU), Idara ya mionzi tiba (Radiotherapy), Idara ya utawala (administration), Idara ya Ushauri na Nasaha (CTC na VTC).
Hata hivyo Hospitali iliweza kupokea jumla ya Tsh. Tsh.1,670,000,000 ambapo Tsh 500,000,000.00 ni Ruzuku ya serikali kuu na Tsh. 1,170,000,000.00 ni Mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa mradi kupitia “Force Account”.
Hadi sasa kituo hicho kimeweza kutumia kiasi cha Shilingi 1,315,578,000.42 na kubakiwa na kiasi cha Tsh 354,578,000.42.
Kupitia utekelezaji wa Mradi huo wenye lengo la kuboresha sekta ya Afya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Eng, Juma Hamsini amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambapo utakapo kamilika utaenda kutoa matokeo chanya katika upatikanaji na utoaji wa huduma ya Afya katika Jiji hilo.
PICHA: MUONEKANO WA JENGO LA OPD COMPLEX KATIKA HOSPTALI YA JIJI LA ARUSHA PINDI UJENZI WAKE UTAKAPO KAMILIKA.
PICHA: MUONEKANO WA UJENZI WA JENHO LA OPD VOMPLEX UKIENDELEA KATIKA HOSPTALI YA JIJI LA ARUSHA ILIYOPO KATA YA ENGUTOTO KATIKA AWAMU YA KWANZA.
MAKALA HII IMEANDALIWA NA LUCAS MYOVELA - MOTIVE MEDIA TANZANIA- 0763 420 108.
Comments
Post a Comment