MGOMO WA KUFUNGA MADUKA WATINGA ARUSHA.

WAFANYABIASHARA WALIA NA VIONGOZI WAO KUUNGANA NA WAHUNI KUITISHA MGOMO.


WAMTAKA RC MAKONDA AFIKE KUOKOA JAHAZI BAADA YA VIONGOZI WAO KUTOKOMEA NA KUWAACHA NJIA PANDA.

Na Lucas Myovela - Arusha.


Ikiwa leo ni siku ya 3 toka kutokea kwa mgomo wa kutofungua maduka kwa wafanyabiashara wa Dar es Salaam mnano Juni 24, 20204 na kisha Juni 25, 2024 Majiji  ya Mbeya na Mwanza na Leo Juni 26, 2024 ni Jiji la Arusha.


Taarifa za awali za mgomo wa leo katika Jiji la Arusha ulianza na taarifa za chini kwa chini kwa kutembeza vipeperushi kwenye kila duka la Jiji la Arusha ambapo vilitaka kila mmliki wa duka kutofungua biashara ili kuungana na wenzao wa mikoa mingine waliyotangulia kufunga.


Mapema leo wananchi wa Jiji la Arusha pasipo kujua hili wala lile wamekutana na mgomo ambao wao walikuwa hawana taarifa nao huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha kungilia kati swala hilo huku wakimlaumu Mbunge wa Jimbo hilo kukaa kimya baada ya kuona vuguvugu hilo likiendelea mikoa mingine na kutofika kwa wanyabiashara kwa wakati.


Ikiwa leo Juni 26, 2024 ikiwa ni siku ya tatu ya kikao kati ya serikali na wafanyabiashara Nchini kikiendelea ila hadi sasa wafanyabiashara hao wamekuwa wakiendelea na mgomo kila kuitwapo leo.

KIPEPERUSHI KILICHOKUWA KINATEMBEA DUKA KWA DUKA ARUSHA AMBACHO KINAKANWA NA KILA KIONGOZI WA WAFANYABIASHARA KUKIJUA.

Jambo hili hadi sasa habari inapokwenda hewani viongozi wa wafanyabiashara Mkoa wa Arusha wamepoteana licha ya wao kuwa vinara wa shughuli hiyo ya momo waliyo iratibu kwa mujibu wa wamiliki wa maduka.


"Kiukweli jana nililetewa kipeperushi na aliyekileta simjui ila aliacha ujumbe mkali sana kuwa kesho ukifungua usilaumiane na viongozi, ila kwakuwa niliulizia nikajua siyo mimi pekee ilibidi nikae kimya ila naamini swala hili viongozi wa Mkoa wanajua maana hata vipeperushi vinasema tuungane na wenzetu waliyotangulia kugoma". amesema mmoja wa wafanyara amabae hakutaka jina lake litajwe.


Hata hivyo kwa upande wa wafanyabiashara wengine waliyojikuta wamewahi kufungua maduka yao wanadai kuwa walifatwa na kuletewa maneno na baadhi ya viongozi na wamiliki wa maduka wenzio kwa kile walichodai wanawasaliti katika mgomo huo.


"Kwakweli sisi wenyewe hatujui tumefunga biashara zetu kwa ajili ya nini na kwamaslahi ya nani waliyo itisha mgomo huu ni wahuni na viongozi hawataki kuongea lolote wala hawataji sababu za mgomo sasa nao niwahuni". alisema mmoja wa wafanyabiashara. 


Miongoni mwa maneno yalipo kwenye kipeperushi hicho ni kulalamikia faini ya Shilingi milioni 15 kwa kosa la kuto kutoa risiti.


Maeneo mengi ya Jiji la Arusha Maduka yaliyofungwa ni Kariakoo, Stendi ndogo, Bondeni, Stendi Kubwa, Ranger Safari's, Samunge, kilombero, Kaloleni, Soko kuu la Arusha n.k.

Hadi hivi sasa viongozi wa wafanyabiashara wamegoma kuongea chochote juu ya mgomo huo na kueleza kuwa hawapo tayari kusema chochete na kauli yao kubwa nikuwa wanadai hata wao hawajui mgomo huo wala hawamjui aliye itisha mgomo huo.














Comments