MOTO KUWAWAKIA BODI YA WANDHAMINI WALIYO TAFUNA MALI ZA WAUMINI ARUSHA.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Wakala wa Usajili ,ufilisi na Udhamini nchini Tanzania (RITA) imeanza kushughulikia mgogoro wa muda mrefu kwa taasisi ya dini ya kiislamu Arusha ya Muslims Union kwa kuunda tume itakayochunguza ubadhilifu wa mali za taasisi hiyo, uliyopelekea waumini wa taasisi hiyo kutokuelewana na kupelekana mahakamani.

Akiongea na waumini wa dini hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Arusha leo Juni 13.2024, Kikao hicho kiliwahusisaha watendaji wa wilaya hiyo, Afisa Mtendaji mkuu wa RITA, Ndg, Frank Kanyusi Frenk.


Ambapo Kanyusi alieleza kuwa  lengo la ujio wake ni kutatua mgogoro huo iliyodumu kwa muda mrefu baada ya kupata taarifa kuwa katika taasisi hiyo kumekuwa na ubadhilifu mkubwa wa mali za waumini.

Kanyusi ambaye pia ni Kabidhi wasii Mkuu wa Serikali, ameeleza kuwa katika kikao cha kwanza baina yake na wadhamini wa bodi hiyo, waumini na wanachama wa taasisi hiyo kilichofanyika Machi 14, 2024 walibaini kwamba bodi hiyo ilikuwa ikifanyakazi kinyume cha sheria kwa kuwa muda wake ulikuwa umeisha.


"Katika kikao hicho tulibaini malalamiko ya wanachama yalikuwa na ukweli na bodi ya wadhamini muda wake ulikuwa umekwisha,na kukubaliana kuunda kamati ya mpito itakayokuwa na majukumu ya kufanya marekebisho ya katiba na kuitisha uchaguzi wa viongozi ,pia kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya taasisi hiyo"


Alisema kamati ya mpito ilikabidhiwa majukumu mbalimbali ikiwemo kuandaa taarifa ya mapato na matumizi hata hivyo ilileta taarifa ya yenye dosari na hivyo kumlazimu Kabidhi wasii mkuu wa serikali kuunda tume mpya ya mpito itakayochunguza migogoro wa taasisi hiyo kwa muda wa siku 14 na kutoa majibu.


"Mimi kama Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa sheria ya muunganiko wa bodi ya wadhamini, natakiwa kuunda kamati ya uchunguzi ili kujiridhisha zile tuhuma dhidi ya bodi ya wadhamini za kutumia vibaya mali za taasisi za taasisi ya Arusha Muslims Union zina ukweli na tayari nimeunda kamati hiyo itakayofanyakazi kwa siku 14 na kuleta majibu"


Kanyusi ambaye pia anasimamia bodi za mpira vyama vya siasa , alisema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakao bainika kutumia vibaya mali za taasisi hiyo na kutoa onyo kwa wadhamini wa bodi zote nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria huku wakijua kwamba mali hizo sio zao ni mali za wanachama.


Pia alisema migogoro ndani ya taasisi mbalimbali za dini hapa nchini bado ni kubwa na anaangalia namna sahihi ya kutatu migogoro hiyo ikiwemo kutoa elimu.


Katika hatua Nyingine Kanyusi aligoma kuzungumzia mgogoro wa taasisi hiyo na baraza la waslamu Tanzania Bakwata kuhusu mali zinazogombewa akidai suala hilo hilo lipo mahakamani na hawezi kulizungumzia na kiwataka waumini hao kusubiri maamuzi ya mahakama.


Baadhi ya waumini wa taasisi hiyo ya Arusha Muslims Union, Azizi Bashiri na Mustafa Kihyago waliishukuri RITA kwa kushughulikia migogoro katika sekta ya dini hatua ambayo itasaidia kudumisha amani .


Hata hivyo waliiomba serikali kua galia namna ya kuwasogezea karibu huduma za Kabidhi wasii Mkuu wa Serikali ili waweze kupeleka malalamiko yao kuliko kusubiri kiongozi mkuu wa Rita kutoka makao makuu kuja kusikiliza kilio chao.



Comments