MRADI WA SEQUIP ULIVYO INUA ELIMU YA TANZANIA.

WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII,SERIKALI IMETIMIZA MIUNDOMBINU YA ELIMU NCHINI.

Na Lucas Myovela -Arusha..


Wanafunzi wamehimizwa kusoma kwa bidii kwa kuwa Serikali imefanya jukumu lake la kuboresha miundombinu ya shule kwa kujenga miundombinu inayokidhi vigezo vya shule vinavyoweka mazingira rafiki ya kusomea na kujifunzia.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava wakati alipotembelea na kufungua baadhi ya majengo katika shule ya Sekondari Mringa iliyopo katika Halmashauri ya Arusha vijijini ( Arusha Dc ).


Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenge shule mpya maabara, vyumba vya madarasa vya kutosheleza, maabara zinazozingatia watoto wenye mahitaji maalum.


"Tumeshuhudia majengo mazuri pamoja na mabweni mazuri ya wasichana inaonesha namna serikali inawajali, niwatake wanafunzi kusoma kwa bidhii ili kurejesha na kumridhisha Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan". Amesema Mnzava


Akisoma taarifa ya Mradi, Mkuu wa shule ya sekondari Mringa, Mwl. Salim Magaka amesema kuwa, mradi huo umetekelezwa na Serikali kupitia miradi ya SEQUIP kwa gharama ya shilingi milioni 260 kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi mabweni.


Aidha amemshukuru Mhe.Rais kwa kuajali watoto wa kike na lujenga mabweni ambayo licha ya kupandisha kiwango cha taaluma zaidi, mabweni yanawahakikishia usalama pamoja na kupunguza mimba na ndoa za utotoni.


"Mazingira rafki ya kusomea na kujifunzia yanaturahisishia kazi hata sisi walimu kazi ya kufundisha na yanamrahisihsia mwanafunzi tendo la kujifunza" Amesema Mwl. Magaka Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu".




Comments