MWENGE WAZINDUA KITUO CHA MAFUTA CHA PUMA.

UJENZI WA KISASA WA SHERI HIYO WAGHARIMU MILIONI 590.

Na Lucas Myovela - Arusha.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndugu Godfrey Eliakim Mnzava ameweka Jiwe la Msingi mradi wa uuzaji wa mafuta kituo cha Puma kata ya Oloirien mapema leo Julai 20, 2024 Mradi huo ambao umeanza kutoa huduma unategemea kugharimu kiasi cha shilingi milioni 590 mpaka kukamilika kwake.


Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, kwa niaba ya mmiliki wa Kituo hicho Yusuf Hure, amesema kuwa mradi huo licha ya kutoa huduma ya mafuta kwa jamii na kuwaingizai kipato umeweza kuajiri watu 27, kuchangia pato la halmashauri na Serikali kwa ujumla wake.


Aidha, ameishukuru Serikalia ya awalu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa hapa nchini.


Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu".


Comments