WAHASIBU WAKUU WA SERIKALI KUTOKA NCHI 54 ZA AFRIKA KUKUTANA ARUSHA.

KUJENGA IMANI YA UUMA KATIKA MIFUMO YA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA KWA UKUAJI ENDELEVU KATIKA NCHI ZA AFRIKA.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Mkutano Mkuu wa Pili wa wahasibu Wakuu wa Serikali Afrika unatarajia kufanyika Jijini Arusha Desemba 2 hadi 5 mwaka huu na lengo kuu ni kuwakumbusha wahasibu katika masuala yao ya kazi ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya fedha yanayozingatia uwazi kwa maslahi ya Umma.

Mhasibu Mkuu wa Serikali, Leornad Mkude. 

Hayo yalisemwa leo Jijini Arusha na Mhasibu Mkuu wa Serikali, Leornad Mkude wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa Mkutano huo utakuwa na washiriki 2000 kutoka nchi 54 za Afrika.


Mkunde ameeleza kwamba Mkutano huo wa pili unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Mkoani Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC kuanzia tarehe 2 hadi 5 ya mwezi Disemba 2024 unalengo la kujenga imani ya umma katika usimamizi wa fedha za umma kwa ukuaji endelevu.

"Lengo kuu la Mkutano wetu huu wa pili ni kujadili mambo mbalimbali na lengo kuu ni Kujenga imani ya umma katika mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwa ukuji endelevu (Building Public Trust in PFM Systems for Sustainable Growth)." Amesema Mkunde.


 "Washiriki wa mkutano huu na walengwa wakubwa ni Wahasibu, Wakaguzi wa hesabu, wataalamu wa masuala ya fedha, Tehama, Vihatarishi kada nyingine wakiwemo waliyo ajiriwa serikalini, makampuni binafsi pamoja na waliyoko katika ajira binafsi". Amesema Mkude.

Aidha Mkude alisema wahasibu na wakaguzi watafundwa katika uwajibikaji na usimamizi bora na matumizi ya fedha yenye kuzingatia taratibu na misingi ya fedha ili kujenga Imani kwa Umma katika kusimamia Mifumo ya Usimamizi wa fedha za Umma.


"Faida za Mkutano huu wa Wahasibu wakuu wa serikali Afrika ni pamoja na kuwa na Afrika yenye mafanikio yenye wa ukuaji jumuishi na maemdeleo endelevu, Bara jumuisshi lililounganishwa kisiasa na kwa kuzingatia maadili ya Pan- Africanism na maono ya mwamko wa Afrika". Ameeleza Mkude.


"Afrika yenye utawala bora, demokrasia, kuhesshimu haki za binadamu na utawala wa sheria, Afrika yenye Amani na usalama, Afrika yenye utambulisho thabiti wa kitamaduni, urithi wa pamoja, maadili na maadili yanayoshirikiwa". Amesisitiza Mkude.

Mkude alisema watakaohudhuria Mkutano huo watapata fursa ya kusikiliza mada za masuala mbalimbali ya kitaalamu, pia kukutana na wahasibu wakuu wa serikali wa Afrika na kubadilishana mawazo,kupeana mawasiliano na kujua fursa nyingine katika nchi za Kiafrika.


"Katika kuunga mkono dhamira ya Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii wetu wa Tanzania, wagni hawa watatembezwa katika kwenye mbuga za wanyama na vituo mbalimbali vya utalii na tunategemea watavitangaza vivutio vyetu katika nchi zao". Ameeleza Mkude.


Aidha Mkude ametoa wito kwa wahasiku, wakaguzi wa hesabu kuweza kuhudhuria mkutano huo muhimu na mlamewataka maafisa masuuli wa Wizara na Taasisi zote kuwaruhisu wahasibu na wakaguzi watakaoomba kuhudhuria Mkutano huo.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika, Malehlohonolo Mahase, alisema kuwa kufanyika kwa Mkutano huo nchini Tanzania kunatokana na Serikali ya Tanzania kuwa na mifumo mizuri ya ukusanyaji kodi,uwazi wa matumizi ya fedha za Umma kwa wananchi na wahasibu wengine kuiga mfano wa Tanzania.


Alisema kuwa mashiriki makubwa ya fedha Duniani kama vile Benki ya Dunia na IMF yamekuwa yakisisitiza umuhimu wa matumizi bora ya fedha yenye kuzingatia maadili ya utumiaji hivyo ni wajibu wetu kukumbushana kwa hilo katika Mkutano huo wa siku tano.


Mahase alisema sababu nyingine ya Mkutano huo kufanyika Tanzania ni pamoja na serikali ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya kitalii na nchi kuwa na utulivu na amani hivyo ni wakati wa nchi nyingine kujifunza kwa hilo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano (AICC), Christine Mwakatobe alisema kuwa wao kama Taasisi wamejiandaa kikamilifu kuwapokea wageni katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuweka kila kitu sawa kwa lengo la kuwavutia wageni hao ili kunufaika na huduma zote katika Mkutano huo.


Mwakatobe alisema AICC kwa sasa iko vizuri katika Utalii wa Mikutano hivyo kuwataka wadau wengine wa ndani na nje kufanya Mikutano katika Kituo hicho kwani kina huduma zuri na za kisasa.





Comments